Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Bw Ban Ki-moon amesema “uvamizi” wa Palestina na udhalilishaji wa Wapalestina lazima ukomeshwe kwa njia ya makubaliano baina ya Waarabu na Israeli.

Taarifa hiyo ilitolewa na afisa mwandamizi wa UN kutokana na kushindwa kwa baraza la usalama la UN kuchukua hatua dhidi ya mauaji ya Israel wakati wa kuadhimisha siku ya Nakba. Siku hiyo iliadhimishwa na Wapalestina siku ya Jumatatu kwa maandamano kukumbuka miaka 63 tangu kuanzishwa kwa utawala wa Israel.

Kwa mujibu wa msemaji wa Ban Ki-moon, Katibu Mkuu huyo alisisitiza umuhimu wa kuwa na ufumbuzi wa amani na haki bila ya kuchelewa, unaohakikisha haki inatendeka kila upande na amani inarejeshwa baina ya Waarabu na Waisraeli.

Hii ni pamoja na kukomesha kwa uvamizi wa ardhi ya Wapalestina na haki ya wakimbizi kurudi makwao, alisema
Majeshi ya Israeli yaliripotiwa kuua si chini ya Wapalestina 10 na kuwajeruhi zaidi ya 110, wakati walipoandamana kusini mwa Lebanon siku ya Jumapili.

Siku hiyo maelfu ya Wapalestina waliandamana wakilaani nchi yao kuporwa tarehe 15 Mei 1948.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: