Mlinzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Tabora, Mohamed Rashidi aliyenusurika kuuawa na wanafunzi wa shule hiyo amesomewa shitaka la wizi huku akiwa katika wodi ya majeruhi hospitali ya Kitete mkoa Tabora ambako anaendelea na matibabu.
Upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Janeth Sekule umedai mbele ya Hakimu mkazi mwandamizi wa Tabora, Issa Magori kuwa Mtuhumiwa Mohamed alitenda kosa hilo mei 11 majira ya saa tano usiku.
Imedaiwa kuwa siku hiyo mtuhumiwa akiwa na mwenzake Idd Shaban ambaye hivi sasa ni marehemu wote wakiwa walinzi wa shule hiyo walivunja ghala la shule kwa nia ya kuiba, lakini walidhibitiwa na wanafunzi.
Mtuhumiwa ambaye amekana shitaka lake bado amelezwa katika wodi namba moja ya hospitali ya mkoa akiendelea na matibabu ya majeraha aliyopata kutokana na kipigo alichokipata kutoka kwa wanafunzi.
Wakili wa Serikali Janeth Sekule ameiambia mahakama hiyo kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi mei 30 mwaka huu, itakapoanza kusikilizwa kwa mara ya kwanza.

Toa Maoni Yako:
0 comments: