Hatimaye kundi la Morogoro Youth Universe of Talents (MYUT) limefanikiwa kubeba bendera ya mji kasoro bahari katika mashindano ya Serengeti Dance la Fiesta ambalo limemalizika katika ukumbi wa For Stars Club mjini hapa. Kikundi hicho ambacho kilionyesha umahili mkubwa wa kucheza hakina itatambulisha vyema mji huo.Ushindani na ubunifu ulikuwa wa hali ya juu.Watu waliojitokeza kuhudhuria Serengeti Dance la Fiesta.Majaji wa Serengeti Dance la Fiesta kutoka kulia ni B-12, Mtangazji wa Clouds Fm 88.4 jijini Dar es Salaam, anafuatiwa na Msami kutoka Tanzania House of Talent pamoja na muandaaji wa kipindi cha ‘Step Up Player’ cha Clouds Tv, Isakwisha Thomson.Kikundi cha Myuti kikitambulishwa. Katika hatua ya kwanza makundi yapatayo manne yamejitokeza kupambana na kutapatikana kundi moja litakaloshinda na kuwakilisha mkoa wa mji kasoro bahari katika mashindano ya Serengeti Dance la Fiesta litakalohitimishwa jijini Dar es Salaam.Kikundi cha Gentlemen kikionyesha umahili wake wa kudance.Kikundi cha Moro Squred wakionyesha umahiri wake katika kudance.

Kikundi cha Kabolate nacho kikiwa tayari baada ya kumaliza kukamua.Mratibu wa mashindano haya Serengeti Dance la Fiesta, ambaye ni mkuu wa vipindi kutoka redio Clouds Fm 88.4 jijini Dar es Salaam, Sebastian Maganga (kulia) kulia akiweka mambo sawa pamoja na Mtangazaji wa redio Clouds Fm Ruben Ndege ambaye ni Mratibu wa Serengeti Fiesta Freestyle.Watu waliojitokeza kuhudhuria Serengeti Dance la Fiesta.

Mtangazaji wa Clouds Tv, Babu wa Kitaa ambaye pia ni MC wa Serengeti Dance la Fiesta akijjaribu kuwapa maelekezo washiriki waliojitokeza kushiriki katika shindano la kudance ndani ya mji kasoro bahari.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: