Moja ya vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva hatuwezi kumuacha msanii wa bongo fleva Abednego Damian a.k.a Belle 9 mtoto wa Moro ni kijana mdogo lakini mwenye uwezo mkubwa wa kufanya muziki katika kiwango kikubwa na kuwafanya hata wakongwe kuwaacha wakijiuliza maswali ambayo hayana majibu kichwani mwao.

Alizaliwa Septemba 9, 1989 huko mjini Iringa na wakahamia mji kasoro bahari, Morogoro.

Kijana huyu ni msanii wa bongo fleva na ni mwandishi wa muziki anayekubalika pande mbali mbali za Tanzania.


Belle 9 mtoto wa Moro alilieleza jarida la Kitangoma kuwa alianza kujihusisha na muziki wa bongo fleva akiwa na rafiki yake B.J akiwa na kundi lao lililojulikana kwa jina la Moro Zeze lililohusisha Juda, Muddy Gado, D.K, Ray, Chris, Diko, Hard P, Prex na Moki japo halikuweza kudumu na kuvurugika kutokana matatizo ya hapa na pale.


"Kiukweli mafanikio haya niliyonayo sasahivi yalitokana na ujasiri niliokuwa nao baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kwenda studio kurekodi ilibidi tuanze kuwahoji viongozi wetu wa makundi na ndipo nilipoonekana mtovu wa nidhamu na ndipo nipofukuzwa," anasema Belle 9.

Aliongeza kuwa kitu subira kinatakiwa katika mambo mengi hapa nikiangalia yote mafanikio yanapatikana kutokana na subira.


Anakumbuka alikutana Mona katika studio za Moro record na kumkutanisha na Abudu Chuma (Tafu AK) na ndipo aliporekodi nyimbo yake ya kwanza aliyojulikana kwa jina la 'Mrembo wa Kiafrika' ambayo haikufanya vizuri na baadae alijitosa tena na kutoa ngoma yake ya pili 'Kaja na Nani' ambayo haikuweza kupenya.


Belle 9 alikutana na Triss akampa ofa ya kurekodi nyimbo na kuamua kurudia nyimbo 'Mrembo wa Kiafrika' ambayo aliona haifai na kuamua kurekodi nyimbo yake ya 'Sumu ya Penzi' ndani ya RocaTZ record iliyopo ndani ya Morogoro.


Sumu ya Penzi ni wimbo ulioweza kumtambulisha vyema kwa mwaka 2008 na kumfanya aweze kupata show nyingi ndani na nje ya Tanzania japo hakusita kusema kuwa Tamasha la Fiesta Jirambe 2008 liliweza nalo kumtangaza vyema na kujikuta akijizolea mashabiki wengi.

Baadae aliweza kurekodi singo yake nyingine ya "Masogange' iliyozidi kumtambulisha vyema na kurekodi albamu yake ya kwanza iliyojulikana kwa jina la 'Sumu ya Penzi' iliyobeba nyimbo 8 ikiwemo, ‘Sumu ya Penzi yanyewe, Umenitupa, Wewe ni wangu, Radha ya mapenzi, Houseboi ambazo nyimbo hizo amezirekodia katika studio mbali mbali.
Alizitaja studio hizo kuwa ni RocaTz Record, Saidi Comorie, More Records ya jijini Mwanza.

Belle 9 hakuweza kuacha kubainisha mambo machache ambayo wasanii wengi huwa wakiulizwa huwa hawapendi kusema, suala hili si lingine ni lile la kutungiwa nyimbo, "Sijawahi kutungiwa na sitakaa nitungiwe nyimbo, namshukuru Mungu kwa kunipa kipaji kikubwa ambacho wasanii wengi hawana, " anasema Belle 9.


Akizungumzia suala la yeye kukosa tuzo la Kili Music Award 2010 na kukanusha juu ya yeye kujitoa katika tuzo hizo, anasema Unajua wasanii wa Morogoro tunafanya mapindizi makubwa sana, japo hatuna bahati ya kupata tuzo. Mimi sijajitoa katika mashindano hayo japo watu wengi walipakaza kuwa mimi nimejitoa, suala la kushindwa ni la kawaida pale wanaposhindanishwa watu wawili.


Belle 9 mtoto wa Moro kwa sasa anajiandaa na albamu yake ya pili na tayari ameanza hivyo wakae mkao wa kula wakati anajiandaa kutoa video yake ya 'Wewe ni wangu'
"Mashabiki wangu kaeni mkao wa kula mambo mazuri yanakuja nitaendelea kuwaletea," ansema Belle 9.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: