Ndugu wananchi

Serikali imepanga eneo la Kilombero kuwa kituo cha kuratibu shughuli za usafiri wa kwenda Loliondo kwa Babu,hii ni katika jitihada za kupunguza magari mengi kule kwa babu. Leo asubuhi kampuni ya kilimanjaro Printers ilikuwa inawalipisha ushuru wa maegesho kwenye eneo hili kinyume na sheria maana serikali ilishatoa tamko kuwa ni kituo tu na hakuna yeyote wa kumtoza yeyote ushuru.

Mimi Diwani nikafanya jitihada na kumkamata huyu wakala na sasa yupo polisi.
Hakuna mwananchi yeyote atakayetozwa ushuru wowote.

Ndugu zangu baada ya kumkamata huyu wakala, ameniletea ilani ya siku 30 ya kukusudia kunipeleka mahakamani kwa kesi ya kumdhalilisha, na kumweka polisi kinyume cha sheria, huu hapa ndio msimamo wangu.

MSIMAMO WANGU KUHUSU ILANI YA SIKU 30 YA KUSUDIO LA KUTAKA NILIPE FIDIA YA 200mil. (MIL. 200)

NDUGU WANANCHI, NA WANAHABARI

Mnamo tarehe 2.4.2011 wakala wa kampuni ya KMPL alikuwa akitoza ushuru wa maegesho magari yaliyokuwa yakiingia katika kituo cha kuratibu safari a loliondo`kinyume cha sheria,kimsingi huyu wakala ana mkataba na halmashauri wa kukusanya ushuru kwenye kituo cha kikuu cha mabasi na si katika kituo hichi cha kuratibu safari za loliondo, kilichopo Kilombero baada ya kupata hizi taarifa za wakala kutoza ushuru niliwasiliana na mkurugenzi wa halmashauri akanihakikishia kuwa hakuna wakala yeyote anayeruhusiwa kutoza ushuru,na ni agizo halali la serikali.

Nilimsihi aondoke kwa kuwa anafanya kazi kinyume cha sheria, lakini alikaidi na kuonyesha madharau, ndipo polisi walipomkamata na kumpeleka kituo kikuu cha polisi. Jana asubuhi nimekuta Ilani yenye Kumb Na NLC/WKL/ARS/02/2011 ya siku 30 Kutoka kwa NOTHERN LAW CHAMBERS ya kukusudia kuishtaki Halmashauri Arusha pamoja na Bwana Nanyaro kwa kosa la kudhalilisha kuharibu mali, na kuwapeleka huyu wakala polisi kinyume cha sheria.Ndugu zangu wanahabari kwanza ni wajibu wangu kama Mhe. Diwani kutetea wananchi na halmashauri hivyo hakuna sheria yeyote niliyovunja kwa kuwazuia huyu wakala kukusanya ushuru, bado nayasimamia maamuzi yangu,na nitayasimamia na nipo tayari kuwajibika kwa kile ninachokiamini, lakini pia namtaka huyu wakala tukutane MAHAKAMANI, kwani ndipo haki hupatikana. Haiwezekani wakala afike kwenye kata aanze kutoza ushuru,bila hata kujitambulisha kwa serikali ya mtaa au ofisi ya kata, bila kuwa na utambulisho wowote, haiwezekani na haikubaliki

Kamwe sitakaa kimya,wananchi wetu waendelee kuonewa. Siogopi wala sitakubali kutishwa na awaye yote katika kusimamia na kutekeleza wajibu wangu kama DIWANI. Na kama anataka msaada wa fedha ili aajiri jopo la mawakili nipo tayari kumchangia.

Napenda niwahakikishie wananchi kwa ujumla kuwa nipo imara, na nitaendelea kuwatumikia kwa moyo wangu wote,na tuendelee kushirikiana kwa ajili ya ustawi wetu sote.

NANYARO J.E.

N:B Kilichoandikwa hapo juu ni kutoka kwa mdau Nanyaro J.E hakijaongezwa kitu chochote wala kuongezwa chochote, naomba wadau msome muone mambo yanavyoendelea Loliondo. Asanteni sana.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: