Spikawa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda(wa nne kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wizara, Idara, Taasisi za Serikali na wakala wa serikali nje ya Ukumbi wa Pius Msekwa mara baada ya kuzungumza nao.Viongozi wengine ni Naibu waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenela Mkangara (wa tatu kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Clement Mshana(wa tano kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Habari,Uhusiano na Elimu kwa Umma Bungeni Bw. Jossey Mwakasyuka(wa pili kutoka kushoto).
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akizungumza na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka nje ya ukumbi wa bunge, leo mjini Dodoma.Katikati ni Naibu waziri wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya Makazi Goodluck Ole Medeye.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda(kushoto) akisalimiana na mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Clement Mshana mara baada ya kuzungumza na maafisa habari, Elimu na Mawasiliano wa Wizara, Idara, Taasisi za serikali, Mikoa na wakala leo mjini Dodoma.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Clement Mshana nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Mh. Jenista Muhagama(katikati) akiongea na maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wizara, Idara, Taasisi za Serikali na wakala wa serikali ndani ya Ukumbi wa Pius Msekwa leo mjini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi na Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Uhusiano na Elimu kwa Umma Bungeni Bw. Jossey Mwakasyuka (kulia).
Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
Toa Maoni Yako:
0 comments: