Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi -Zanzibar
Jeshi la Polisi mkoa wa mjini Magharibi Zanzibar, leo limepokea msaada wa kompyuta moja aina na Dell kutoka Benki ya NMB yenye thamani ya shilingi milioni 2.8 ili kusaidia kuhifadhi kumbukumbu za makosa ya Usalama Barabarani mkoabni humo.
Akipokea kompyuta hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Kamishna Msaidizi (ACP) Aziz Juma Mohammed, amesema kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka kwani Jeshi la Polisi hivi sasa lipo katika mchakato wa kuratibu shughuli zake kwa kutumia teknolojia ya kisasa kama sehemu ya kurahisisha utendaji wa kazi zake.
Kamanda Aziz amesema kuwa kutokana na mabadiliko ya teknolojia ulimwenguni, kopyuta ni chombo cha msaada mkubwa kwa Jeshi la Polisi kwani mbali ya kuhifadhia kumbukumbu lakini pia inaweza kutumika kama njia ya kufanyia upelelezi wa mifumo ya mitandao ya kompyuta.
Amesema hivi sasa wahalifu wengi wamekuwa wakitumia mifumo ya kompyuta kufanikisha mawasiliano na makundi mengine ya kihalifu jambo ambalo amesema kama kuna haja kubwa ya Polisi nao kwenda na wakati.
Kamanda Aziz ameishukuru Benki ya NMB na kuyaomba Mashirika na Benki nyingine hapa nchini kama sehemu ya wadau kuangalia uwezekano wa kulisaidia Jeshi la Polisi kupata vifaa ili liweze kuboresha utendaji kazi wake kwa jamii.
Kwa upende wake, Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar, Bw. Mluku Abdallah Maggid, amesema kuwa NMB imeamua kutoa msaada huo ikiwa ni hatua ya Benki hiyo katika kuunga mkono jitihada za Jeshi la Polisi katika kuihudumia jamii kwa ukaribu zaidi.
Aidha Bw. Maggid ametoa wito kwa Taasisi na Mashirika mengine hapa nchini kuona umuhimu wa kulisaidia Jeshi la Polisi hasa ikizingatiwa kuwa Serikali pekee haiwezi kulifanya Jeshi hilo kufikia malengo yake ya kupambana na uhalifu katika Nyanja zote.
Kompyuta hiyo ya kisasa iliyotolewa na NMB itatumika katika kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa mjini Magharibi Unguja katika kusaidia kuhifadhi kumbukumbu za makosa ya Usalama Barabarani.

Toa Maoni Yako:
0 comments: