*Mkuu wa Mkoa kufungua Michezo

Timu ya Netiboli ya Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu-Dodoma (CDA) itapambana na timu ya Ukaguzi kutoka Dar es Salaam ikiwa ni moja ya mechi za ufunguzi za michuano ya Michezo ya Mei Mosi Taifa itakayoanza tarehe 16 April, 2011 kwenye Uwanja wa Jamuhuri mjini Morogoro.

Katika mechi nyingine ya ufunguzi kwa upande wa Mpira wa Miguu, Timu ya Kikapu ya kukausha na kusindika tumbaku (TTPL) ya Morogoro itapambana na Timu haki za Binadamu na Utawala Bora kutoka jijini Dar es Salaam.

Pamoja na michezo hiyo kuanza tarehe 16 Aprili, 2011 Mkuu wa mkoa wa morogoro, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya (Pichani) anatarajiwa kuyafungua rasmi mashindano hayo mnamo tarehe tarehe 18 Aprili, 2011.

Jumla ya Timu 23 kati ya 33 zilizoalikwa tayari zimethibitishwa kushiriki kwenye michezo ya mwaka huu ambayo itashirikisha michezo ya mpira wa miguu, Netiboli, Kuvuta kamba, Riadha, Kuendesha Baiskeli, Bao, Drafti na Karata.

Miongoni mwa Timu zilizothibisha ni pamoja na mabingwa watetezi wa mwaka jana 2010 kwa upande wa mpira wa miguu na Netiboli, Wizara ya mambo ya ndani.

Nyingine zilizothibitisha ni ofisi ya Waziri Mkuu, Ukaguzi, Uhamiaji, Wizara ya Maliasili na Utalii, Kampuni ya kuchambua na kukausha tumbaku (TTPL), mamlaka ya ustawi Makao Makuu-Dodom (CDA), Tume ua Utumishi wa Umma, Wizara ya uchukuzi, ofisi za wakuu wa mikoa ya Rukwa, Dodoma na Iringa, Shirika la Mzinga, Halmashauri ya mji wa Kilosa, Wizara ya Ulinzi, Polisi Makao Makuu, Hazina, mMhakama Kuu ya Tanzania, Ofisi ya Raisi- Mipango, Wizara ya Afya, Haki za Binadamu na Utawala Bora na Chuo cha Mipango (IRDP)-Dodoma.

Timu zote zilizothibitisha kushiriki zinatakiwa ziwe zimefika Morogoro tarehe 14 April, 2011, Viongozi wawili wa kila timu (Mwenyekiti na Katibu) watatakiwa kuhudhuria mkutano wa mwisho kabla ya michezo kuanza utafanyika kwenye uwanja wa Jamhuri kuanzia saa 4 kamili asubuhi ambao baadae saa 9 alasiri utafuatiwa na mkutano mwingine utakaohusisha michezo ya timu zote shiriki.

Timu ambayo itakuwa imechelewa na michezo wake kupangwa kwenye ratiba na kusababisha mchezo kutofanyika itakuwa imepoteza mcehzo huo. Hivyo timu zote zinahimizwa kufika Morogoro mapema tarehe iliyopangwa.

Kauli Miu ya Michezo ya Mwaka huu ni "Serikali Iwatupie Macho Viongozi Makazini Wasiopenda Michezo"

Imetolewa na: Award Safari
Katibu Mkuu
Kamati ya Michezo ya Mei Mosi Taifa.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: