Mashindano ya ulimbwende ngazi ya kitongoji kanda ya kaskazini, Miss Arusha City Center 2011 yanatarajiwa kufanyika mei 13 mwaka huu katika Club ya Tripple A, jijini Arusha.

Akizungumza na gazeti hili, mraribu wa shindano hilo Bi. Sophia Urio alisema kuwa kwa sasa wamejiandaa vyema tayari kwa ajili ya kufanya mashindano hayo.

Shindano hilo linalotarajia kufanyika katika jijini Arusha tayari mpaka sasa wameshakamilisha mchakato wa kuwasaka warembo na watahakikisha Miss Tanzania wa mwaka huu wanatokea mkoani Arusha.

"Tunamshukuru Mungu kwa maandalizi ambayo tumeshayafanya mpaka sasa, tunachosubiri kwa sasa ni uzinduzi wa mashindano hayo ili tuweze kuendelea na kila kitu," alisema Bi. Sophia Urio.

Mashindano hayo ambayo yanatarajia kuwakutanisha warembo 10 hakika yatakuwa ya kupendeza sana maana mwaka huu kuna mabadiriko makubwa na mafanikio mengi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: