Kiongozi wa bendi ya African Stars International 'Twanga Pepeta', Luiza Mbutu (kushoto), akiongea jambo kwa wanahabari, kulia ni mratibu wa shindano hilo Maimartha Jesse.
SHINDANO la kumsaka Kimwana Manywele Twanga Pepeta 2011, limewadia ambapo warembo wataanza kuchuana rasmi mei 6 mwaka huu ndani ya ukumbi wa Sun Cirro.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, mratibu wa shindano hilo, Maimartha Jesse, alisema kuwa mshindi atakayepatikana kwa mwaka huu atazawadiwa Duka la Vipodozi lenye thamani isiyopungua shilingi milioni tano, (5,000,000/=), ambalo pia litakuwa wilaya ya Kinondoni.
Maimartha aliongeza kuwa, duka hilo litalipiwa kodi na leseni ya mwaka mzima bila kuainisha jina la mmiliki maana atakuwa hajafahamika kwa wakati huo.
Warembo hao wanatarajiwa kuingia kambini kuanzia jumanne ijayo kwa ajili ya mazoezi, ambayo watajifua chini ya kiongozi wa wanenguaji wa Bendi hiyo Kassim Mohamed 'Super K'.
Picha na Mussa Mateja / GPL
Home
Unlabelled
SHINDANO LA KIMWANA MANYWELE TWANGA PEPETA 2011 LAJA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments: