Dkt Antony Mwandulami akitoa kikombeWakazi wa Iringa na vitongoji vyake wakiwa wamefulika kupata kikombe.

Na Francis Godwin, Iringa

WAGONJWA Iringa, Mbeya na Vuruma leo wamiminika nyumbani kwa Dkt Antony Mwandulami (58) mkazi wa kijiji cha Itunduma Wangama wilaya ya Njombe mkoa wa Iringa kupata dozi ya bure ya vikombe vitatu vya dawa kama ya babu wa Loliondo.

Huku wagonjwa waliokunywa na kupona washuhudia kuwa kikombe hicho sio kama cha Mbeya ni kama Loliondo.

Wakitoa ushuhuda wa kikombe hicho akiwemo Nery Kasoli (50) mkazi Mbeya mjini ambaye alikuwa na binti yake Hilda Asenga (30)aliyekuwa asumbuliwa na kichaa na kutoa ongea kwa muda mwingi ambaye sasa amepona.

Alisema kuwa binti yake huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo kwa muda wa miaka takribani 10 ila baada ya kupata kikombe mtoto wake huyo amepona na anazungumza vizuri kabisa.

Huku Issa Omary (45) yeye alidai kuwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na kutibiwa katika hospitali mbali mbali za seikai bila mafanikio ila baada ya kunywa kikombe hicho hali yake ni nzuri na juzi amekwenda kupima Hospitali ya Ikonda ameonekana ni salama.

Wengine waliotoa ushuhuda wao jana ni pamoja na kijana mmoja ambaye alijitambulisha kwa jina moja la Kevin ambaye anadai kuwa alikuwa akisumbuliwa na HIV ila sasa amepima na kuonekana ni salama.

Akizungumza na waandishi wa habari waliofika nyumbani kwake kushuhudia zoezi hilo la utoaji wa dozi ya vikombe vitatu ,Mwandulami alisema kuwa lengo la kuanza kutoa bure dawa hiyo ni kutaka wagonjwa kutoa ushuhuda zaidi wao baada ya kunywa dawa hiyo badala ya vyombo vya habari na watoa huduma hiyo kuendelea kujitangaza zaidi na kujisifia kwa jambo ambalo si geni.

Mwandulami ambaye ni mshauri mkuu wa waganga wa tiba asilia Tanzania ameanza kutoa kikombe hicho ijumaa ya wiki iliyopita na kudai kuwa mti huo hajaotoshwa na Mungu wala mizimu bali alionyesha na marehemu baba yake zaidi ya miaka 18 sasa amekuwa akiutumia miti huo aina ya Makhirikhiri kwa kuchanganya na miti mingine.

Hata hivyo Mwandulami yeye amekuwa akitoa dozi hiyo kwa kutumia kikombe cha udongo huku kikombe cha Plast amekuwa akitumia kugawia dawa hiyo ambayo huiweka katika ndoo kubwa ya lita 60 huku kwa sasa wagonjwa wakipewa dozi hiyo bila malipo yoyote.

Kwani tayari amepata kutumia dawa hiyo kwa muda mrefu sasa kutibu wagonjwa waliokuwa wakisumbuliwa na magonjwa sugu na tayari wengi wao wamerudi kushukuru baada ya kupona na kuwa bado anaendelea na uchunguzi ili kujua kama kweli dawa hiyo inaweza kutibu UKIMWI kabla ya kuutangazia umma.

“Naomba sana wagonjwa wangu wanaofika kupata kikombe ambao wanatumia dozi za UKIMWI kwa sasa kuendelea kutumia dozi hizo...hadi serikali itakapo tuma timu ya madaktari kuja kuchunguza dawa hii na kujua idadi ya magonjwa inayotibu kama na UKIMWI upo”

Mwandulami alisema kuwa bado anapenda kuikumbusha serikali kuwa makini na utitiri wa vikombe vinavyoendelea kutolewa na kuwa wengi wao ni matapeli ambao wanafanya hivyo kwa ajili ya kujipatia utajiri wa haraka haraka na sio kuhudumia jamii kama ilivyokwake na babu wa Loliondo.

“Mimi huyu babu wa Loliondo ni kama amenifunua kwa kiasi japo mimi na yeye bado mimi ni mkongwe zaidi yake na uhuhuda wa wagonjwa wanaofika kupata tiba hapa na wale waliopatiwa tiba ni ukweli zaidi ya wale wa Loliondo ambao hata miezi mitatu haijamalizika….mimi hapa nimeanza kutoa huduma hii miaka zaidi ya 17 sasa ila ambacho nilikuwa nikikosea mimi ni kuchanganya na miti mingine ndio maana wagonjwa walikuwa wakipona kwa kasi ndogo ila toka ijumaa nilipoanza kuchemsha mtii huu peke yake mafanikio makubwa nimeyaona kwa wagonjwa sugu kupata nafuu”

Hata hivyo alisema kuwa dawa yake hiyo haina masharti yoyote zaidi ya mgonjwa kufika na kunywa japo mambo ya msingi kama ya ulezi wa kupindukia na uzinzi si vizuri kwa mgonjwa kuendelea nayo kwa kipindi cha dozi hiyo.

Pia aliishauri serikali kupitia wizara ya afya kutuma wataalam wake kwake na maeneo mengine ambayo vikombe hivyo vimeibuka ili kuchunguza mti huo na uhaali wa dawa hiyo kama ina sifa kama ile ya Loliondo na kuiruhusu kusindikwa katika chupa ili wagonjwa wengi waweze kuipata pale walipo popote nchini badala ya kutumia gharama kubwa kusafiri hadi Loliondo ama kuja Wilayani Njombe .

“Huu ni wakati wa matapeli kujiinua na kama serikali haitakuwa makini na kubariki haraka haraka kama ilivyo kwa kijana wa Mbeya basi kuna uwezekano wa watanzania kuendelea kupoteza muda wao na kuibiwa na watu hao ambao baadhi yao wameibuka na kudai sasa wanatibu kwa majani ya mahindi jambo ambalo ni utapeli wa wazi"

Pia alisema kuwa dawa hiyo ambayo amekuwa akiitoa inaweza kuhamishika na mgonjwa sehemu yeyopte nchini anaweza kuipata na kuwa mtabibu ambayo anadai kuwa dawa yake haihamishike kama babu wa Loliondo ni wazi kuwa kuna mkono wa ushirikina katika utoaji wa huduma hiyo.

“Hivi Mungu alipomtuma Mwanaye Yesu kristo kuja duniani kuwakomboa wanadamu wote ni sio wa kabila na koo ana mkoa Fulani …..Kwani Mungu alimtuma Yesu kuifanya kazi hiyo sehemu moja peke ….mbona alizunguka mijini na vijijini kuwahubiria injili wanadamu wote bila ubaguzi …sasa huyo babu anataka kusema Mungu wake yeye ni yupi ni Mungu wa wanadamu wote ama ni Mungu wa Loliondo pekee” alihoji Mwandulami

Mwandulami alitaka watanzania kupima na kuchuja mambo kabla ya kuamini na kuwa ni wakati mzuri sasa kujiuliza maswali juu ya vikombe hivyo na kuwapuuza wanaodai kuwa vikombe havihamishiki wakati wao wamehamisha mizizi toka porini hadi katika makazi yao.

Alisema dawa yake imekuwa ikitibu kwa siku tatu baada ya kumaliza dozi ya vikombe vitatu ambapo kila mwezi ni kikombe kimoja na kuwa kwa sasa bado hajapanga ni kiasi gain kwa mgonjwa aweze kulipia ila mbele ya safari kila kikombe kitakuwa shilingi 2000.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: