NI kituko chenye sura ya aibu kwa tabaka la mastaa, inaelezwa kwamba wengi wao hawapendi kuvaa ‘kufuli’ a.k.a kabati (nguo ya ndani) kwa maelezo kuwa zinawanyima uhuru.

The Udaku Master, Ijumaa limethibitisha hilo baada ya wao wenyewe kukiri kwamba hawavai kufuli kwa sababu mbili, mosi ikiwa ni biashara ili kuwatega midume, pili ni kukimbia mistari ambayo hujichora kwa nje.

Nyota wa Shindano la Bongo Star Search 2008 (BSS Season 2), Baby Joseph Madaha amesema kuwa, anafagilia kwa sana staili ya kutovaa kufuli kwa sababu inamuweka huru.

Baby alisema, anajichia bila kufuli kwa sababu yeye siyo staa wa kwanza Bongo kutovaa nguo hiyo muhimu kwani wengi tu hawavai.

“Hii staili inaitwa komando. Ni nzuri sana, mimi sipendi kujibana ndiyo maana sivai. Hapa Bongo mastaa wengi wanafagilia staili hiyo, hata mamtoni (Marekani, Ulaya) akina Paris Hilton na Britney Spears mara nyingi hawapendi kuvaa nguo hiyo,” alisema Baby.

Mbali na Baby, mastaa wengine watatu waliozungumza na Ijumaa, walikiri kuwa waumini wa kutovaa kufuli, ingawa waliomba wasiandikwe gazetini.

“Mimi sivai kabisa, yaani nikiwa kwenye mitoko yangu bila hiyo nguo, najiona nipo huru sana. Nimuogope nani?” Alihoji mmoja wa mastaa hao ambaye anatisha kwenye fani ya mitindo.

Mmoja wa wakali wa filamu Bongo alisema: “Mwanzoni nilikuwa navaa nguo ya ndani lakini baada ya kucheza filamu mbili, niligundua mastaa wengi hawavai, kwa hiyo na mimi niliacha.

“Tukiwa tunabadilisha nguo wakati wa kurekodi filamu ndiyo niligundua wengi hawavai, nilipouliza, wengi waliniambia zinawabana na kuwafanya wakose uhuru, hivyo na mimi sivai tangu wakati huo, sana sana navaa taiti.”

Mbali na hao, mastaa wengine waliozungumzia tabia hiyo ya kutovaa kufuli ni hawa;

HUSNA IDD ‘SAJENT’
Aliliambia gazeti hili kuwa tabia ya mastaa wengi kutovaa kufuli anaijua, ingawa yeye haipendi.

“Nimeshasikia hiyo tabia ya mastaa kutovaa nguo za ndani. Nawajua wengi hawavai lakini mimi siipendi,” alisema Husna ambaye alitoka mshindi pili wa Shindano la Kimwana Manywele wa Twanga Pepeta mwaka 2007.

AUNT EZEKIEL ‘GWANTWA

Alisema: “Naijua hiyo tabia kwa sababu nimeshasikia kwamba mastaa wengi hawavai nguo za ndani lakini mimi hata siku moja siwezi kuetembea ‘mkavu’.”

ROSE NDAUKA
Alisema: “Kusema ukweli mimi sijawahi kusikia kama kuna mastaa wanaokata mitaa bila ya kuvaa nguo za ndani, ila mimi kwa kweli siwezi kutoka nyumbani bila kuvaa hiyo nguo.”

JAQUELINE PATRICK
Alisema: “Ni kweli kuna mastaa hawapendi kuvaa nguo za ndani kwa kuhofia kukaa vibaya na kutoa mistari kwa nje lakini mimi nashauri wawe wanatafuta zile nyepesi kwa sababu haziwezi kuonesha.”

ELIZEBETH MICHAEL ‘LULU’

Alisema: “Hiyo staili ya komando ndiyo kwanza naisikia. Mimi siwezi kutoka nyumbani bila kuvaa nguo ya ndani.”

WEMA SEPETU
“Nimeshasikia kwa mastaa wa nje ambao wanatoka bila kuvaa nguo za ndani, hapa Bongo sijawahi kusikia na kwa upande wangu navaa kama kawaida. Sidhani kama naweza kutembea bila kuvaa nguo ya ndani,” alisema Wema.

JAQUELINE PENTEZEL ‘WA CHUZ’
“Hiyo mbona siyo ‘ishu’? Kuna mastaa wengi sana ambao hawavai nguo za ndani. Labda wanatafuta biashara lakini mimi sipendi kuacha kuvaa. Nawashauri bora wajitahidi kuvaa hata bikini kuliko kutovaa kabisa,” alisema Jack wa Chuz.

SHAMSA FORD
Alisema: “Jamani, mimi nashangaa sana. Hivi kweli inawezekana mtu kutembea bila kuvaa nguo ya ndani? Kwa kweli mimi siwezi.”

BELINA MGENI
Alisema:”Tabia hiyo ipo kwa baadhi ya mastaa ila mimi siifagilii. Kutembea bila kuvaa kufuli ni sawa na uchuro, wasiovaa kama kweli wanataka kuheshimika basi wabadilike.”

KUTOKA KWA MHARIRI

Gazeti hili linawaomba mastaa wa kike kujiheshimu na kuvaa mavazi ambayo hayawezi kuwafanya wakatafsiriwa tofauti ikiwa ni pamoja na kuvaa kwa staha.

ZAIDI NA ZAIDI ANGALIA HAPA
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: