TATARIFA YA MKUTANO WA MHE.MIZENGO PETER PINDA
WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA UTAKAOFANYIKA TAREHE 26 SEPTEMBA 2010 SAA 9
MCHANAWAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA UTAKAOFANYIKA TAREHE 26 SEPTEMBA 2010 SAA 9
----
Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,New York,unapenda
kuwaarifu ndugu Watanzania wote wanaoishi katika maeneo yaliyotajwa na
pia ya jirani kuwa Mhe.Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter Pinda yupo
mjini New York kwa shughuli za kikazi ambapo pamoja na mambo mengine
atahudhuria mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa(UNGA)
akimwakilisha Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Wakati wa ziara hiyo angependa kukutana nanyi Watanzania siku ya
Jumapili tarehe 26 Septemba,2010.Mkutano huo utafanyika kuanzia saa
9 mchana hadi saa 11 jioni.Mnaombwa kuhudhuria.
MAHALI AMBAPO MKUTANO UTAFANYIKA NI:
Nyumba ya Mheshimiwa Balozi Mwanaidi Maajar
30 Overhill Road
MT. VERNON,
NY 10552
Toa Maoni Yako:
0 comments: