
Meneja wa Sheir Illusions, Susan Miseda akitoa taarifa ya ujio wa msanii mahiri katika miondoko ya Salsa, Joush Tasia Rhumba kutoka nchini Ireland kwa waandishi wa habari waliofika katika ukumbi wa mikutano wa Paradise Hoteli.Msanii huyo atawasili hapa nchini kwa ajili ya shoo moja itakayofanyika tarehe 2,oktoba katika hoteli ya Hilton,jijini Dar.kushoto ni Mkurugenzi wa Kijiji cha SOS CHILDREN'S TANZANIA,Dr. Alex Victor Lengeju.

Mkurugenzi wa kijiji cha kulea watoto waishio katika mazingira ma gumu (SOS CHILDREN'S TANZANIA) Dr. Alex Lengeju akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari namna ya uendeshaji wa kijiji hicho.kulia ni Meneja wa Shear Illusions,Susan Miseda.
------------------------------ MSANII mahiri wa muziki wa Salsa kutoka nchini Ireland, Joush Tasia Rhumba, anatarajiwa kutoa burudani katika hafla maalum ya kuchangia fedha kwa watu wasiojiweza ‘Blast from the past Shear Charity Ball 2010’ itakayofanyika Oktoba 2 hoteli ya Double Tree by Hilton, iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo ambayo imeandaliwa na taasisi ya Shear Illusions, itaambatana pia na uzinduzi wa jarida la ‘Shear Hair and Beauty Magazine’ lililopo sokoni kwa mwaka mmoja sasa, ambako mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mbunge mteule wa Bumbuli, January Makamba.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa hafla hiyo, Suzan Miseda alisema kwamba, tamasha hilo la hisani litakuwa likifanyika kila mwaka, ili kutambua mchango wa kuaminika wa wateja wa jarida hilo na kuwahamasisha wapya kuhusu kujiunga na familia ya Shear.
Alisema, mapato yatakayopatikana katika tukio hilo yataelekezwa katika mfuko wa taasisi ya CCBRT, ambao hutunisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye ulemavu na tatizo la fistula, ambalo wahanga hufanyiwa upasuaji bure katika taasisi hiyo.
“Sehemu nyingine ya mapato hayo yatakwenda kwa ‘SOS Children’s Village’, kusaidia maisha ya watoto yatima na waliotelekezwa, ambao hulelewa katika kituo hicho kinacholea watoto wakiwa katika makazi maalum yaliyo kama kijiji,” alisema.
Aidha, Suzan alisema kwamba, ili kushiriki katika hafla hiyo, kutakuwa na tiketi maalum zitakazouzwa kwa shilingi 150, 000 kwa kila meza, huku tamasha hilo likibeba ujumbe wa ‘60’s, 70’s na 80’s, ambako wageni wote watatakiwa kuvaa magauni mazuri yatakayoendana na ujumbe huo.
Hafla hiyo imedhaminiwa na Vodacom Foundation, NBC, Pure Academy, Benchmark Productions, Darling, NSSF, Advertising Dar, Sam’s Super Store Ltd, Moss & Plants, Tinamaria Boutique, Clouds Tv & Radio, Colosseum Hotel, S.S. Concrete Company Ltd, CCBRT, Shear Illusions, I- View Media, Paradise City Hotel na Double Tree by Hilton Hotel.
Toa Maoni Yako:
0 comments: