Waziri wa Mambo ya Nje Mh. Bernad Membe akizungumza na waandishi wa habari katika makao Makuu ya Wizara hiyo jijini leo juu ya mkutano wa 14 wa AU uliofanyika kuanzia Februari 1-2/ 2010 jijini Adis Ababa nchini Ethiopia, ambapo mkutano huo ulimchagua Rais wa Malawi Bingwa wa Mutharika kuwa Mwenyekiti mpya wa AU baada ya Rais Muamar Gadafi wa Libya kumaliza muda wake.

Waziri Bernad Membe amesema katika mkutano huo pia Rais Alli Bongo wa Gabon alichaguliwa kuwa makamu wa kwanza wa AU na pia ukamchagua Rais Yoweri Museveni wa Uganda kuwa makamu wa pili wa AU.

Ameongeza kuwa mambo mengine yaliyojadiliwa katika mkutano huo ni suala zima la mfumo wa Mawasiliano katika bara la Africa ICT Information Communication Technology, masuala ya Usalama kama vile Sudan, Guinea, Madagascar na Somalia na suala la Somalia Tanzania na Misri zimekubali kutoa mafunzo kwa maafisa wa usalama 1000 wa Somalia kutoka makundi mbalimbali ya wababe wa vita nchini humo,pia akasema suala lingine liliojadiliwa ni mabadiliko ya Tabia nchi (Climate Change) kushoto aliyeko katika picha ni Kaimu katibu mkuu wa Wizara ya Mambo ya NjeBalozi Mohamed Mzale.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: