Wakazi wa Msasani Bonde la Mpunga eneo la Maandazi Road jijini Dar, leo walikumbwa na hofu kubwa baada ya mtu asiyejulikana kulitelekeza bomu kwenye kichochoro kimoja mtaani hapo.Afisa Mtendaji wa Mtaa huo Bi. Rose Temu, alisema kijana mmoja alionekana mtaani hapo akitafuta mtu wa kumuuzia bomu hilo kama chuma chakavu lakini wanunuzi walionesha wasiwasi kuwa huenda ni bomu ndipo kijana huyo aliamua kulitelekeza mtaani hapo.Kufuatia tukio hilo kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania, kikosi maalum cha kutegua mabomu, kilifika eneo la tukio na kulichukua kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi. Mengi zaidi gonga hapa
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: