Ofisi ya rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma, imewapiga mkwala waandishi wa habari kutosogeza kabisa pua zao karibu na mnuso wa harusi la rais Zuma linalofanyika leo.
Ofisi ya rais imewatahadharisha waandishi wa habari kwamba, shughuli hii ni ya kifamilia zaidi ya udaku wa kidunia. Zuma anafunga ndoa leo na atakayekuwa mke wake wa tano, Bi. Thobeka Madiba (37), anayetoka vijiji vya KwaZulu-Natal.
Pia Madiba amekuwa akitokea katika minuso kibao ya kiofisi na Rais Zuma. Gazeti la Sunday Times la huko bondeni limedai kwamba kuna hekaheka kibao za sherehe zinaendelea katika makazi ya Rais kwa ajili ya harusi hilo. Maturubai makubwa yameezekwa kwa ajili ya wageni waalikwa, na hadi tunakwenda mitamboni mbuzi na ng'ombe kadhaa walikuwa wamesharudisha namba ili wageni washibe.
Zuma kwa sasa ni baba wa watoto 18 na pia ana mchumba mwingine, Gloria Bongi Ngema kutoka Durban. Hakuna mwenye habari kamili ndoa yao itakuwa lini.

Rais Zuma alikwisha lipa mahari, inayojulikana kwa jina la ilobolo, kwa familia ya Madiba mnamo mwaka 2007. Kwa sheria ya Afrika Kusini ni kwamba Zuma na Madiba ni kama wameshaona tayari, na hata hivyo wana watoto watatu waliozaa pamoja.
Pia Madiba amekuwa akitokea katika minuso kibao ya kiofisi na Rais Zuma. Gazeti la Sunday Times la huko bondeni limedai kwamba kuna hekaheka kibao za sherehe zinaendelea katika makazi ya Rais kwa ajili ya harusi hilo. Maturubai makubwa yameezekwa kwa ajili ya wageni waalikwa, na hadi tunakwenda mitamboni mbuzi na ng'ombe kadhaa walikuwa wamesharudisha namba ili wageni washibe.
Inasemekana pia kwamba wanakijiji wa karibu na linapoangushwa harusi hilo nao watajimuvuzisha kushiriki katika suala zima la upigaji wa vigelegele.
Kwa Zuma huyu anakuwa ni mke wake wa tano sasa ukiacha Sizekele Kuhumalo na Nompumelo MaNtuli-Zuma. Pia aliwahi kumuoa na kumtaliki Nkosazana Dlamini-Zuma ambaye ni waziri wa mambo ya ndani wa Bondeni kwa sasa. Kate Mantsho Zuma, ni mke mwingine ambaye alijiua mwaka 2000.
Kwa Zuma huyu anakuwa ni mke wake wa tano sasa ukiacha Sizekele Kuhumalo na Nompumelo MaNtuli-Zuma. Pia aliwahi kumuoa na kumtaliki Nkosazana Dlamini-Zuma ambaye ni waziri wa mambo ya ndani wa Bondeni kwa sasa. Kate Mantsho Zuma, ni mke mwingine ambaye alijiua mwaka 2000.
Zuma kwa sasa ni baba wa watoto 18 na pia ana mchumba mwingine, Gloria Bongi Ngema kutoka Durban. Hakuna mwenye habari kamili ndoa yao itakuwa lini.
Tunamtakia kila la heri rais Jacob Zuma katika harusi yake. Kuoa raha, hasa kama uwezo wa kuwatunza wake zako haukupi tabu.
Jadili habari hii kwa kubofya hapa
Habari imetayarishwa na libeneke la Fotobaraza kwa hisani ya News24.com

Toa Maoni Yako:
0 comments: