Askofu Zakaria Kakobe katikati akiongoza wafuasi wake kupinga Tanesco kupitisha nyaya za umeme mkubwa katika kanisa lao.
TANESCO wamekanusha kuwa na nia mbaya na wafuasi wa kanisa la Gospel Bible Fellowship Church (GBFC) lililo chini ya Askofu Zacharia Kakobe kufuatia tuhuma za wafuasi hao kwamba TANESCO inataka kuwaharibia kanisa lao.
TANESCO wamekanusha kuwa na nia mbaya na wafuasi wa kanisa la Gospel Bible Fellowship Church (GBFC) lililo chini ya Askofu Zacharia Kakobe kufuatia tuhuma za wafuasi hao kwamba TANESCO inataka kuwaharibia kanisa lao.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam leo, Afisa habari msaidiszi wa TANESCO, Chaby Barasa amesema lengo lao ni kutaka kuimarisha mfumo wa umeme na kusaidia upatikane kwa urahisi wakati wote.
“Hatuna nia yakuwaharibia kanisa wafuasi wa GBFC isipokuwa ni kwa nia njema kwani ni wakati muafaka sasa maeneo yote yapate nyaya madhubuti ili kusaidia kupunguza matatizo ya umeme katika maeneo mbalimbali,” alisema BarasaKwa upande wake mchungaji Zacharia Kakobe amesma wataendelea kuweka kambi kulizunguka kanisa lao ili kuhakikisha kuwa TANESCO hawafanikishi zoezi lao.
Mchungaji Kakobe ametamka rasmi kuwa yeye pamoja na wafuasi wake wako tayari kufa na si kuachia kanisa libomolewe na kupitishwa nyaya.Mgogoro huu bado ni mzito kati ya TANECSO na wafuasi wa GBFC kwani mpaka sasa wafuasi hao wanalala nje ya kanisa mpaka hapo itakapoamuliwa vinginevyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: