Wapendwa wadau wa Habari na Matukio, ni matumaini yangu kuwa ni wazima kabisa na mnaendelea vyema na shughuli zenu za kila siku.

Kwanza kabisa tunapaswa kumshukuru Mungu ambaye ni muumba wa mbingu na ardhi pamoja na vyote vilivyomo ndani yake kwa kutujaalia afya njema katika kipindi kizima cha mwaka 2009 na tuzidi kumuomba kwa kila hali ili aweze kutujaalia zaidi na zaidi katika kipindi kijacho cha mwaka 2010 na kuendelea, kwani yeye ndiye muweza wa yote.

Wadau wangu Habari na Matukio inapenda kuchukua fulsa hii kwa siku ya leo kutoa salamu zangu za dhati kwenu ikiwa ni katika kipindi cha msimu wa sikukuu ya Krismas na huku tukijiandaa kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2010 ambao siku chache tu zijazo tutakuwa tumeshaufikia.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: