D'banj kutoka Nigeria.
Mwanamuziki mahiri kutoka Nigeria, anayetamba na singo zake kali kama Fall In Love, Olorun Maje, Gbono Fele, Entertainer , Suddenly, na Igwe, Dapo Daniel Oyebanjo maarufu kwa jina la D’banj, anataraji kukandamiza shoo moja matata siku ya Jumamosi ya Novemba 28, 2009 katika viwanja vya Tanganyika Parkers (Kawe).
Wasanii wengine watakaoporomosha burudani sambamba na mkali huyo ni Juacali, Nonini na Nameless wote kutoka Kenya.
Tanzania itawakilishwa na wakali TID, Mangwea, Belle 9, Cpwaa, kundi la THT, Marlaw, Joh Makini na Quick Racker.
Burudani hiyo itaporomoshwa chini ya udhamini wa Str8Musics mahsusi kwa ajili ya Wanachuo wote.Shoo inataraji kuanza mishale ya saa 11 jioni na kumalizika saa 8 usiku.
Toa Maoni Yako:
0 comments: