Hili ni eneo la mbele yalipokuwa makazi ya kifalme nchini China . Hapa wanaonekana wenyeji na wageni mbalimbali wakimiminika kwa wingi kutembelea eneo la makumbusho linalojulkana kama Forbidden City ambalo enzi za utawala wa kifalme haikuruhusiwa kwa mtu yeyote kuingia.
Kundi la vijana wapatao 50 kutoka Tanzania wakiwa na raia wa nchi hiyo pamoja na raia wa nchi mbalimbali waliofurika kutazama jumba la makumbusho mahali walipoishi wafalme 24 wa China mahali panapojulikana kama “ Forbidden City ”. Eneo hilo kwa sasa limetengwa kwa ajili ya makumbusho na watu wanaokadiriwa milioni sita hutembelea eneo hilo kwa mwaka.
Vijana kutoka Tanzania Bw. wakiongozwa na ofisa mipango wa Idara ya Kimataifa ya Chama cha vijana nchini China Ding Jiaming wakijiandaa kuingia katika eneo linalojulikana kama Forbidden City ambalo zamani lilitumika kama makazi ya wafalme nchini China . Eneo hilo llikuwa maalum kwa ajili ya makazi ya wafalme na familia zao tu na hakuruhusiwa mtu yeyote kuingia katika eneo hilo lakini kwa sasa baada ya kumalizika kwa utawala wa kifalme linatumika kama makumbusho ambapo watu wengi hufika a kujionea ufundi mkubwa uliotumika katika ujenzi wa makao hayo ya kifalme.
Mfanyakazi wa kituo cha makumbusho cha Beijing ( Beijing Planning Exhibition hall) Bi. Cindy Wang akitoa ufafanuzi kwa kundi la vijana kutoka Tanzania kuhusu historia ya kale ya mji wa Beijing.Takribani vijana wapatao 50 wako nchini China kwenye ziara ya mafunzo kufuatia mwaliko wa rais wa nchi hiyo Hu Ji ntao alioutoa kwa rais wa Tanzania Jakaya Kikwete Februari mwaka huu.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: