”Hongera Wazanzibari kwa ushindi wa Copa Coca Cola”

Chama cha Wananchi (CUF) kimeupokea ushindi wa timu ya vijana wa Mkoa wa Mjini Magharibi katika mashindano ya Copa Coca Cola kwa furaha na fakhari kubwa. Huu ni ushindi wa Zanzibar na Wazanzibari wote na dalili kwamba nchi yetu ina vipaji vingi vyenye uwezo wa kulifanyia makubwa taifa hili, ikiwa tu vipaji hivyo vitapatiwa nafasi.

CUF inachukua fursa hii kuwapongeza vijana wetu hawa kwa kuiwakilisha vyema nchi yetu katika mashindano hayo na kutujengea heshima ya hali ya juu kitaifa na hata kimataifa. Jukumu la kuwaendeleza vijana hawa ni letu sote na hivyo ni vyema sasa tukashirikiana kuona kwamba katika mashindano ya siku zijazo, ushindi huu unaendelezwa.

CUF inawataka vijana wetu nao wasiridhike tu kwamba mara hii wamekuwa washindi, badala yake waendeleze moyo huu wa ushindi, washiriki mazoezi kila siku na wazidishe nidhamu katika michezo, kwani hiyo imekuwa ndiyo siri ya ushindi.

Pamoja na salamu za Chama

Imetolewa na:

Salim Bimani
Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma
CUF
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: