Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya a.k.a bongofleva Juma Nature ambaye pia ni kiongozi wa kundi la TMK Wanaume Halisi lenye makazi yake Temeke jijini Dar, anatarajia kuzindua albamu yake machi 20 katika ukumbi wa Diamond jubilee jijini Dar.

Juma Nature ambaye inaelezwa kuwa ni msanii pekee aliyewahi kuvunja rekodi ya kujaza ukumbi wa Diamond jubilee kuliko msanii yeyote wa hapa yumbani, anazindua albamu yake itakayoitwa TUGAWANE UMASKINI yenye jumla ya nyimbo 11.

Albamu hiyo ambayo kwa sasa iko sokoni,imesheheni ladha mbalimbali ili kuifanya iwe bora na yenye kukubalika kwa kiwango kikubwa,aidha baadhi ya nyimbo zilizomo humo ni siku ya wiki,ulevi,tugawane umaskini,Afrika no 1,kukaa nyumbani,Lakavunda,mgeni wa nani na nyinginezo. Albam alizowahi kuzindua ni NIni Chanzo,Ugari,Ubin adam kazi,History,na sasa hii ya Tugawane umaskini.

Kwa yeyote atakae hitaji nakala/albamu ya TUGAWANE UMASKINI aidha CD ama TAPE wala usisite.

Wasiliana nao kwa namba hizo hapo chini.
0787 878108
0713 424943
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: