Kutoka ndani ya sanaa ya muziki wa Injili, msanii Flora Mbasha ameiambia safu hii kwamba, anatarajia kuzindua albamu mpya ya video za nyimbo zake yenye jina la ‘Furaha yako’, siku ya Sikukuu ya Pasaka ikiwa ni zawadi kwa wapenzi wa kazi zake.

Staa huyo wa Injili alisema kuwa, sehemu kubwa ya maandalizi ya uzinduzi huo imeshakamilika na siku chache zijazo atalitaja eneo la tukio itakapofanyika shughuli hiyo.

“Nawaomba wapenzi wa nyimbo zangu na muziki wa Injili kwa ujumla wasikose kununua albamu hiyo ya video pamoja na ‘audio’ yake ili wapate kusikia maneno mazuri ya kumtukuza Mungu niliyoongea ndani ya kazi hizo,” alisema Mbasha ambaye bado anaendelea kutamba na nyimbo zake mbalimbali katika fani hiyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: