Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete ametoa msaada wa vyakula kwa vituo vya kulelea watoto yatima, wazee, walemavu na wasiojiweza ili waweze kusherehekea vyema sikukuu ya Iddi Mubaraka.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Rais Kikwete kwa viongozi wa vituo hivyo Mnikulu Rajabu Kianda alisema kuwa wametoa vyakula kwa vikundi kumi ambapo viwili ni kutoka Tanzania Visiwani na nane kutoka Tanzania Bara.

Kianda alisema kuwa ni kawaida ya Rais Kikwete kutoa kutoa vyakula kwa vikundi hivyo kila wakati wa sikukuu unapowadia ili kuwafanya nao wajione ni watu wa kawaida kama wengine na kusherehekea sikukuu hiyo kwa furaha zaidi.

“Kila kipindi cha sikukuu Rais anachagua vikundi kumi na kutoa msaada wa chakula ambapo kwa sikuu hii ya Idd Mubaraka vikundi vilivyopata msaada ni Nunge, Dar – Arqam, VOSA, Makao ya Furaha, Chakuwama, Tua Moyo Hosteli, Chuo cha Ufundi kwa wenye ulemavu na Kurasini vyote vya jijini Dar es Salaam”.

“Kwa upande wa Tanzania Visiwani vituo viliyopewa msaada huo ni Mabaoni Chakechake Pemba na Forodhani Zanzibar”, alisema Kianda.

Nao viongozi wa vikundi hivyo walimshukuru Rais Kikwete kwa moyo wake wa upendo kwao na kumtakia maisha mema ili aweze kuwasaidia na wahitaji wengine.

Vituo hivyo vimepata msaada wa Mchele kilo 100, mbuzi wawili na mafuta ya kupikia ndoo moja ya lita 20 kwa kila kituo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: