Chama cha walimu mkoani RUVUMA (CWT) kimeanza kuendesha kampeni ya kuwahamasisha walimu wa mkoa huo kushiriki katika mgomo wa walimu wa nchi nzima uliopangwa kufanyika kuanzia Oktoba 15 mwaka huu.

Mwenyekiti wa CWT mkoani humo Bwana CASTORY NGONYANI amesema kampeni hiyo inalenga kutoa maelekezo juu ya namna ya kuendesha mgomo huo na kuimarisha msimamo wa chama.

Alisema mkoa wa RUVUMA wenye walimu 6729 unadai shilingi milioni 712 kutoka serikalini ikiwa ni sehemu ya madai ya shilingi bilioni 16.4 wanazodai walimu wote hapa nchini kutokana na malimbikizo ya mishahara, likizo na uhamisho pamoja na madai mengine saba yahusuyo maslai ya walimu.

Baadhi ya wakazi wa RUVUMA walizungumza na Habari na Matukio wameitaka serikali kulipa haraka deni hilo la walimu kabla ya kuanza kwa mgomo huo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: