MAJAMBAZI wanne wakiwa na bastola na silaha za jadi, wameteka gari la abiria na kuwapora abiria katika kijiji cha MWADA wilaya BABATI mkoani MANYARA Kamanda wa Polisi wa mkoa wa MANYARA

BW. LUTHER MBUTTU amesema tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 7:00 asubuhi katika barabara ya MBULU- ARUSHA, ikilihusisha gari lenye namba za usajili T 898 ADM TOYOTA LAND CRUISER iliyokuwa na abiria 14.

Kamanda Mbuttu amesema abiria mmoja anayesadikiwa kuwa jambazi aliomba kuteremka katika eneo la shule ya sekondari MBUGWE, na kuomba afunguliwe mlango wa nyumba ili achukue mzigo wake, ghafla majambazi wengine watatu waliibuka kutoka kichakani na kulivamia gari hilo.

Amesema licha ya kufanya uporaji huo, majambazi hayo ambayo mpaka sasa hayajakamatwa, yalifyatua risasi moja hewani kisha yakawajeruhi kwa kuwapiga rungu kichwani, dereva wa gari hilo Bw. DEOGRATIAS LEONARD (30) na abiria mmoja

BW. GAUDENCE TEMU.Amesema katika tukio hilo, majambazi hao wamewapora abiria mali kadhaa, zikiwemo fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 3, simu za mikononi na kisha yakaondoka na gari hilo likiwa na abiria na mizigo yao kurejea Mbulu na kulitelekeza gari hilo katika kijiji cha MASWARE baada ya kuhisi yanafuatiliwa na polisi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: