Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipandisha bendera ya chama baada ya kuzindua ofisi mpya ya tawi la CCM Chuo Kikuu Tumaini.
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema Chama cha CCM na Serikali yake visilaumiwe moja kwa moja kwa mapungufu ya mtu mmoja mmoja kwa sababu vyombo vyote hivyo viwili ni safi.
Alikuwa akizungumza eneo la Kihesa mjini Iringa leo (Ijumaa Mei 2, 2008) wakati wa uzinduzi wa tawi la CCM la Chuo Kikuu cha Tumaini na kutoa kadi kwa wanachama wapya 700.
Tuhuma kuhusu rushwa na wizi ni kwa mtu mmoja mmoja ambaye atakuwa na mapungufu yake, lakini siyo kwamba ni sera ya Chama na Serikali yake.
"Chonde chonde, nihukumuni mimi Pinda kwa yale ninayokosea…Muondoeni Pinda kama ni tatizo lakini chama kiendelee" na Serikali yake kwa vile ni utaratibu wa kujisafisha tu.
Aliongeza: "Chama hiki (CCM) ni kizuri na serikali yake nzuri, kama kuna mapungufu basi yatashughulikiwa na hatua zitachukuliwa."
Akijibu hoja katika risala ya tawi hilo kuhusu ajira kwa wahitimu wapya na kupanua wigo wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo, alisema Serikali itajitahidi kuhakikisha wahitimu hao wanatumika vizuri.
Alisema pia kwamba utaratibu wa mikopo haujapangika vizuri kwa kuwa lazima kwanza kuwajua wote wale wasiokuwa na uwezo wanaohitaji hasa mikopo hiyo.
Hata hivyo Waziri Mkuu alipinga hoja kwamba Serikali imeharakisha kuanzisha vyuo vikuu kadhaa bila ya maandalizi ya kutosha ya uwezo wa kuviendesha.
Hata hivyo Waziri Mkuu alipinga hoja kwamba Serikali imeharakisha kuanzisha vyuo vikuu kadhaa bila ya maandalizi ya kutosha ya uwezo wa kuviendesha.
Alisema nafasi za vyuo vikuu lazima ziongezeke kwa vile usipofanya hivyo basi utakuwa na vijana wengi waliomaliza sekondari gtu na hivyo hilo lityakuwa tatizo kuzwa zaidi.
Waziri Mkuu alizindua tawi la CCM la Chuo Kikuu cha Tumaini katika shughuli iliyopangwa kutekelezwa muda mfupi tu kabla ya kurejea Dar es Salaam kutoka Iringa ambako alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete kwenye sherehe za Mei Mosi kitaifa jana (Alhamisi Mei 1, 2008).
Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu
S.L.P. 3021
DAR ES SALAAM
Ofisi ya Waziri Mkuu
S.L.P. 3021
DAR ES SALAAM


Toa Maoni Yako:
0 comments: