RAIS JAKAYA KIKWETE ameziagiza Shule za sekondari za kata nchini, kuhakikisha kujenga maabara pamoja na kuwahimiza watoto wa jamii ya wafugaji kwenda shule ili jamii iweze kuharakisha maendeleo yake kwa kuwa na wanasayansi na wasomi wendi nchini .
Kauli hiyo aliitoa Rais Kikwete baada ya kuzindua jengo la Shule ya sekondari ya Kizigo iliyopo Wilayani Manyoni.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja wa shule ya sekondari ya Kizigo.

Rais Kikwete amesema kuna haja kwa serikali na wananchi kuongeza jitihada hizo za kuboresha maendeleo ya elimu ikiwemo sekta ya sayansi ambayo ndio msingi katika ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi nchini.
“Tuna hitaji kubwa la wahandisi, madaktari na wataalam mbalimbali na hatutapata watu wa aina hiyo kama shule hizi zitaendelea kuwa bila maabara, kwa hali hiyo, nitumie fursa hii kuwaomba mfanye kila njia ili maabara yenye vifaa vyote muhimu, yapatikane”,alisema.
Rais Kikwete amesema mbali na kuboresha kitengo cha sayansi lakini pia kuna umuhimu wa kuangalia uwezekano wa kuongeza mabweni katika shule hizo za Kata ili ziweze kuwasaidia wanafunzi wanaoishi mbali na hata kuwaepushia na vishawishi mitaani vitakavyoweza kuharibu maendeleo ya elimu zao.
Hatahivyo baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo Bwana Braze Yohane, story Mwanzalima na Therina Wilfred wamesema kuwa kuna umuhimu wa kuchukua hatua za haraka za uhamasishaji wa elimu katika Wilaya hiyo ambayo bado inahitajika jitihasa za ziada za kuelimisha umma kuhusu elimu kwa motto.
Katika hatua yingine, Rais Kikwete amesema serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika sekta binafsi na za kidini ili kuimarisha ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi nchini .
Kauli hiyo ameitoa baada ya kuzindua nyumba 10 za kuishi za watumishi wa afya katika Hospitali ya St. Gasper inayomilikiwa na Kanisa Katoliki lililopo katika tarafa ya Itigi Wilayani Manyoni.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Singida Bwana Parseko Kone katika taarifa yake, amesema Mkoa unakabiliwa na upungufu mkubwa wa madaktari bingwa na wataalam mwengine wenye ujuzi wa masuala ya afya.
Hivi sasa kuna jumla ya watumishi 934 kati ya mahitaji halisi 1636 ya watumishi wa kada mbalimbali, Kwa hiyo mkoa una upungufu wa watumishi 702 ambayo ni sawa na aslimia 43 ya mahitaji halisi.

Toa Maoni Yako:
0 comments: