Lile sakata la ushirikina limezidi kurindima tena katika jiji la Dar es Salaam, ambapo leo asubuhi wananchi walijazana Kituo cha Polisi Kawe kumuona Kingwelu Buruma Kaunda, ambaye anadaiwa alifariki katika mazingira ya kutatanisha Januari 26 mwaka huu na kuzikwa katika makaburi ya Mwananyamala. Kulikuwa na madai mtu huyo amhifadhiwa kituoni hapo, baada ya kukamatwa akiwa uchi maeneo jirani. Habari hizo bado hazijathibitishwa na zinaendelea kufuatiliwa. (pichani) Ndiye Bw. Kingwelu anayedaiwa kuonekana akiwa hai. Hapa ni enzi ya uhai wake akiwa na familia yake ufukweni mwa Bahari ya Hindi akipunga upepo.
Umati uliofurika kituo cha Polisi ukitaka kumuona anayedaiwa kuwa alikufa na sasa ameonekana akiwa hai.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: