Rais JAKAYA KIKWETE ambaye yupo mjini YOKOHAMA nchini JAPAN kuhudhuria mkutano wa TICAD 4 wenye lengo lakuwahamasisha wajapani kuwekeza katika bara la AFRIKA leo ameshiriki katika shughuli mbalimbali zinazotangulia mkutano huo.

Siku ya leo Rais KIKWETE amekuwa na mazungumzo na Waziri Mkuu wa JAPAN Bwana YASUO FUKUDA ambapowalizumzia masuala ya kuimarisha ushirikiano kati yanchi hizo mbili.

Katika mkutano huo Tanzania na JAPAN imesisitizakuimarisha ushirikiano uliopo kati ya nchi hizo mbiliwakati wa mazungumzo yaliyofanyika leo mchana kati yaRais JAKAYA KIKWETE na Waziri Mkuu wa JAPAN BwanaYASUO FUKUDA.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano huo Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wakimataifa Mheshimiwa BENARD MEMBE, JAPAN imeiomba TANZANIA kupitia wadhifa wa uenyekiti wa Umoja waAfrika wa Rais JAKAYA KIKWETE kuiunga mkono nakuisaidia katika jitihada zake za kutaka kuingiakatika baraza la usalama la umoja wa mataifa ombi ambalo TANZAIA imelikubali.

Rais JAKAYA KIKWETE amekubali ombi hilo na kumtaka Waziri Mkuu wa JAPAN Bwana YASUO FUKUDA kuhakikisha kuwa AFRIKA inapata viti vyake katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Baadaye mchana huu Rais KIWETE alishiriki katika mdahalo ulioandaliwa na Shirika la la Japan linaloshughulikia masuala ya maendeleo la JICA nakuwahusisha viongozi wanchi mbalimbali za AFRICA.

Akizungumza katika mdahalo huo RAIS Kikwete amesema Afrika inahitaji kusaidiwa na nchi zilizendelea kiuchumi kama Japan katika sekta za viwanda, biashara, na kilimo ili kufikia maendeleo ya kiuchumi na kufikiamalengo ya milenia ya 2015.

Alisema hayo jana alipojibu hoja zilizotolewakwenyekongamano la kimataifa kuhusu maendeleo yakiuchumi ya Afrika kutokana na uzoefu wa bara la Asia, ambalo pia lilizungumzia wajibu wa sekta ya umma nabinafsi katika kuchochea maendeleo hayo.

Rais alisema maendeleo hayo hayatasaidia Afrika pekee, bali pia kwa mataifa yaliyoendelea kwa kupata masokoya bidhaa na kuondoa matatizo, yakiwamo ya wahamiajiharamu.

Rais Kikwete amesema uchumi wa nchi nyingi za Afrika unakua, ambapo pia faida kwa wawekezaji ukilinganishana maeneo mengi duniani na kwamba serikali zimewekamazingira mazuri ya uwekezaji.

Akitoa mfano wa TANZANIA Rais KIKWETE amezungumzia fursa za masoko na kusema kwamba bidhaa za umeme namagari zilizopo TANZANIA zinatoka Japan.

Alisema kwa watengenezaji wa bidhaa hizo kuwekezaTanzania, watapata soko na faida kubwa kwa kuwa karibu na walaji.

Kuhusu maeneo yanayohitaji msaada kwaTanzania, alisema ni sekta ya elimu, hususan ujenzi wa maabara kutokana na serikali kwa ushirikiano nawananchi kujenga sekondari nyingi.

Naye Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dk.DonaldKaberuka amesema JAPAN inapaswa kutumia urafiki wakena nchi za AFRIKA kuweka vitega uchumi katika nchihizo ili nazo ziwe na maendeleo makubwa kama nchi zaASIA.

Aidha Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi ameelezakwamba nchi zilizoendelea kama JAPAN zinapaswakusaidia nchi za AFRIKA ili kuepuka matatizoyatakayojitokeza kwa waafrika kama magonjwa na masualaya uhalifu kuathiri nchi zilizoelea pia.

Naye Rais mstaafu wa Msumbiji, Bwana Joaquim Chissanoamesema kwa hivi sasa waafrika wanajituma kufanya kazihivyo wanapaswa kusaidiwa zaidi kwa kuongezewa nguvuna mataifa yenye viwanda vikubwa kama Japan.

Mdahalo huo uliongozwa na Rais wa Shirika la Misaadaya Maendeleo la Japan (JICA), Sadako Ogata ambayealiwashukuru viongozi hao kwa kuwa mstari wa mbelekatika kuhakikisha kwamba masuala ya maendeleoyanafikiwa.angela yokohamaadm
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: