WANANCHI wa Jiji la Mbeya wameigomea Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Jijini Mbeya ya kutaka kuongeza viwango vya bei ya Huduma ya Maji kuanzia Julai mosi Mwaka huu.

Wakiongea katika Mkutano ulioitishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(EWURA) wa kujadili na kutoa maoni yao juu ya maombi ya Mamlaka hiyo, Wananchi hao wamesema kuongeza bei ya Huduma hiyo ni kuwatwisha mzigo mkubwa Wananchi.

Wamesema hawakubaliani na maombi ya Mamlaka hiyo kupandisha Bei ya huduma ya Maji, kwa vile hivi sasa Wananchi wana mizigo mikubwa, ikiwemo ya bei kubwa za Nishati ya umeme.

Wameitaka Mamlaka hiyo itafute vyanzo vingine vya mapato, badala ya kuwabana Wananchi ambao wengi wana kipato cha chini, pia wameiomba Serikali iweke utaratibu wa kutoa ruzuku kwa Mamlaka hiyo ili kuwapa unafuu Wananchi.

Wananchi hao pia wameishambulia EWURA kuwa ni wababaishaji kutokana na kuitisha mikutano ya kukusanya maoni juu ya mapendekezo ya bei mpya za huduma mbali mbali, lakini wakitoa maoni yao hayafanyiwi kazi, na badala yake bei zinaendelea kupanda.

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Jijini Mbeya imetoa mapandekezo ya kuongeza viwango vya bei ya huduma ya maji kwa asilimia 28.49, kwa Wateja wake wote, isipokuwa wale wa Vibanda(Vioski) ambao wameomba kuwaongezea asilimia tano.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: