BAADHI ya Watanzania wanaoishi Marekani, wamesema kashfa ya ufisadi iliyoibuka Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) na Kampuni ya Kuzalisha Umeme wa dharura ya Richmond Development Company LLC, imewadhalilisha.
Katika barua pepe aliyotuma kwa Mwananchi kutoka Jimbo la Carolina kwa niaba ya wenzake, John Mashaka alisema, kutokana na kashifa hizo, wamekuwa wakijiuliza kama wahusika ni wazawa au majambazi kutoka nchi za nje.
Mashaka alisema kutokana na hali hiyo, lazima wahusika wote wakamatwe na isipofanyika hivyo, itakuwa ni kejeli na matusi makubwa kwa walimu, polisi na wafanyakazi wengine wanaofanya kazi katika mazingira magumu.
?Ni jambo la kusikitisha na kutoa machozi, unapowaona watu wachache waliopewa dhamana ya kulinda nchi, wanajaribu kuifilisi na kuchezea jasho la Watanzania wengi, huku watoto wakifa hospitalini kwa kukosa tiba,? alisema Mashaka.
Kuhusu ufisadi, Mashaka alisema unasababishwa na watu kukosa uzalendo na kufanya uamuzi ambao hauna maslahi kwa Watanzania.
?Mtu mwenye ubinadamu katika nafsi yake na mwenye uzalendo na uchungu kwa nchi yake, kamwe hawezi kushiriki vitendo vya aibu kama vile vya Richmond na BoT,? alisema Mashaka.
Akitoa mfano wa Israel, Mashaka alisema nchi hiyo ina uwezo mkubwa kitaaluma kuliko mataifa makubwa yenye uwezo wa uchumi, kutokana na viongozi wake kutanguliza maslahi ya taifa mbele.
Mashaka alisema, Watanazania waishio Marekani, wameridhika na juhudi za Rais Jakaya Kikwete kuboresha maisha ya wananchi na kuweka Tanzania katika ramani nzuri.
Pia, alielezea kuridhishwa na jinsi wabunge wa chama tawala na vyama vya upinzani, walivyoungana na kushirikiana katika sakata la Richmond na kufanikiwa kuwang'oa mafisadi.
Licha ya ufisadi, Mashaka alisema wamefurahishwa na juhudi za serikali kutangaza Tanzania kimataifa hasa vivutio vikubwa vya utalii vilivyopo nchini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: