Mfanyabiashara mmoja wa madini nchini, ameapa kumpata kimapenzi kisha kufunga ndoa na aliyekuwa mshiriki wa Jumba la Big Brother Africa II (BBA II 2007), Tatiana Durao wa Angola.

Kibopa huyo anayemiliki mashimo kadhaa katika mgodi wa Tanzanite, Mererani mkoani Manyara na mwenye jina kubwa katika orodha ya wafanyabiashara wakubwa nchini, amekusudia kutimiza dhamira hiyo mara baada ya mrembo huyo kuwasili nchini hivi karibuni.

Tatiana, atawasili Dar es Salaam tarehe 22, mwezi huu kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwemo maonesho ya mavazi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Muungano pamoja na ufunguzi wa Hoteli mpya ya Naura Springs iliyopo Arusha.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mfanyabiashara huyo (jina tunalo) ambaye anaishi Mbezi Beach, Dar es Salaam, amekuwa akiwatambia washirika wenzake wa kibiashara kuwa ni lazima ampate Tatiana hata kama itamlazimu kutumia robo ya utajiri wake kwakuwa huyo ndiye mwanamke wa ndoto zake.“Dah! Mshirika siku hizi hatulii, tangu aliposikia Tatiana anakuja hapa Bongo, imekuwa tabu kweli kweli.
Kila anachoongea ni kuhusu Tatiana, anasema atahakikisha akifika hapa ni lazima amchukue na baada ya hapo ni ndoa,” kilisema chanzo chetu.Kiliendelea kusema: “Anamsifu Tatiana kwa ucheshi wake, umbo lake na hata sauti yake ambayo mwenyewe anasema inamvutia sana.
Anadai amevutiwa zaidi na sura pamoja na rangi ya mrembo huyo ambayo ina mchanganyiko wa Muafrika na Mzungu.”Kiliongeza kuwa hivi sasa mfanyabiashara huyo amejibatiza jina la utani na anajiita Papa Nyenyere, akimaanisha kuwa atampata Tatiana kwa staili ya kutambaa chini kwa chini kama afanyavyo mdudu nyenyere.
Tatiana aling’ara mwaka jana katika fainali za BBA II na kufanikiwa kushika nafasi ya tatu. Akiwa katika jumba hilo, Muangola huyo alianzisha uhusiano wa kimapenzi na Richard Bezuidenhout wa Tanzania.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: