Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima akizungumza katika Mkutano wa Tume, Wahariri na Waandishi wa Habari, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, Agosti 4, 2025 ambapo amewahakikishia washiriki hao kuwa, ofisi yake itafanya kazi nao kwa karibu katika kipindi cha uchaguzi mkuu kwa njia mbalimbali ikiwemo kushiriki katika vipindi vya redio na runinga na kutoa taarifa kwa wakati. Picha na INEC.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima (Kulia), akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Giveness Aswile, kabla hajafungua Mafunzo ya Wahariri na Waandishi wa Habari, yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, leo Agosti 4, 2025.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Giveness Aswile akizungumza katika Mkutano wa Tume, Wahariri na Waandishi wa Habari, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, Agosti 4, 2025.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima (Katikati waliokaa), Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Giveness Aswile (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Daftari na TEHAMA, Stanslaus Mwita (kushoto), Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria Selemani Mtibora (wa pili kulia), na Mwenyekiti wa Mafunzo ya Wahariri na Waandishi wa Habari, Lilian Timbuka (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahariri na waandishi wa habari baada ya kufunguliwa kwa mafunzo hayo katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, leo Agosti 4, 2025.

Na CathbertKajuna, Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima, amewahakikishia wahariri na waandishi wa habari kuwa tume hiyo itashirikiana nao kwa karibu katika kipindi chote cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Akizungumza Agosti 4, 2025 katika Mkutano wa Tume, Wahariri na Waandishi wa Habari uliofanyika Mlimani City, Dar es Salaam, Kailima alisema INEC itakuwa karibu na vyombo vya habari kwa njia mbalimbali ikiwemo kushiriki kwenye vipindi vya redio na runinga, pamoja na kutoa taarifa kwa wakati.

Alisema ushirikiano huo unalenga kuimarisha uelewa kwa wananchi na kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uwazi na amani.

Mkutano huo umetajwa kuwa sehemu ya mkakati mpana wa INEC wa kuhakikisha uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 unakuwa wa amani, huru na wa haki, huku ikisisitiza kuwa habari zenye mizizi ya ukweli ni silaha muhimu ya kulinda demokrasia ya taifa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: