Baadhi ya Wadau na wafanyakazi kutoka kampuni ya The Net Work inayochezesha mchezo wa Kubahatisha wa Tatu Mzuka wakiadhimisha miaka 56 ya Uhuru kwa kufanya usafi wa mazingira mwishoni mwa wiii katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kawe Beach, Kinondoni jini Dar Es Salaam.
Baada ya kumaliza kufanya usafi wakafurahi kwa pamoja.
Shughuli ya usafi ilifanyika kwa makini kuhakikisha eneo la Fukwe linabaki safi.
Wadau wa Usafi wakijadilaiana jambo. 

Kampuni ya The Net Work inayochezesha mchezo wa Kubahatisha wa Tatu Mzuka mwishoni mwa wiki imeadhimisha miaka 56 ya Uhuru kwa kufanya usafi wa mazingira katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kawe Beach, Kinondoni jini Dar Es Salaam.

Akizungumza wakati wa shughuli hizo za usafi,Mratibu wa mawasiliano kutoka kampuni ya The Net Work inayochezesha mchezo wa Kubahatisha wa Tatu Mzuka ,Kemi Mutahaba amesema kuwa wameamua kufanya usafi kwa kushirikiana na baadhi ya Wadau kwa kujitolea,lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika suala zima la kuboresha usafi wa mazingira yetu.

"Tumejitolea kufanya usafi katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kawe Beach,lengo likiwa ni kutunza mazingira na kuweka mazingira yetu safi, lakini pia ikiwa sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika suala zima la kuboresha na kuyaweka mazingira yetu kuwa safi wakati wote",alisema Kemi.

Kemi alisema yote hiyo ni kuhakikisha wanasimamia mlengo wa kampuni yao,waliounzisha katika suala zima la kusaidia kulinda mazingira,ambapo hivi karibuni walichangia kwa kuikabidhi Serikali kiasi cha fedha milioni 100 ili zitumike katika kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa Kijani kupitia mpango maalum ambao Serikali iliishauandaa.

Amesema kuwa Kampuni yake itaendelea kuunga mkono Serikali kwa kuhakikisha kuwa wanachangia katika shughuli za maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo mazingira.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: