Mkuu wa wilaya ya Kilolo Bi Asia Abdalah akishirikiana na wanafunzi wa shule ya Sekondari Kilolo kufanya usafi wa kufyeka nyasi nje ya ofisi ya mkuu huyo wa wilaya juzi kama sehemu ya kuitikia agizo la Rais Dr John Magufuli la kila jumamosi ya mwisho wa mwezi ni siku ya usafi
Jengo la ofisi la ofisi ya DC Kilolo
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilolo akishiriki usafi nje ya ofisi ya DC Kilolo
Watumishi Kilolo na wanafunzi wakifanya usafi ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Bi Asia Abdalah na wakuu wa idara katika Halmashauri ya Kilolo wakiwa wameungana na wanafunzi wa shule ya sekondari Kilolo kusafisha mazingira yanayozunguka ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kilolo.
Usafi nje ya ofisi ya DC Kilolo.
DC Kilolo akishiriki usafi na wanafunzi wa shule ya msingi Kilolo
DC Kilolo Bi Asia Abdalah akiwa na wanafunzi wa baadhi ya watumishi wa Kilolo walioshiriki usaf
Na MatukiodaimaBlog
MKUU wa wilaya ya Kilolo Asia Abdulah ametangaza kuwachukulia hatua kali wananchi watakaopuuza agizo la Rais Dr John Magufuli na kufanya usafi wa mazingira yanayowazunguka kila juma la mwisho la mwezi.
Huku akipiga marufuku kilimo cha mahindi nje ya ofisi yake kuwa kuendelea kulima mahindi na mazao yanayozidi futi tatu katika eneo linalozunguka ofisi yake ni moja ya uchafuzi wa mazingira na kuwa kuanzia sasa mazao marefu katika maeneo yote yanayozunguka ofisi za umma ni marufuku.
Mkuu huyo wa wilaya alitoa kauli hiyo juzi baada ya kuongoza oparesheni ya usafi kwa watumishi wa Halmashauri ya Kilolo na wanafunzi wa shule ya sekondari Kilolo kufanya usafi maeneo ya jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya ya kilolo jengo ambalo nyoka walikuwa wakitishia usalama wa watumishi wa ofisi hiyo kutokana na jengo hilo kuzungukwa na nyasi ndefu na vichaka kwa zaidi ya
miaka 10.
Akizungumza baada ya zoezi hilo mkuu huyo wa wilaya aliwapongeza wakuu wa idara katika halmashauri ya Kilolo pamoja na wananchi ambao waliitikia wito wa kufanya usafi huku akisema idadi ya wananchi waliofika kufanya usafi hajafurahishwa nao kwani ni wananchi wachache ambao walitoka kufanya usafi pamoja na gari ya matangazo kupita mitaani kabla ya siku ya usafi na kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi hilo.
“Wakati nikifika wilayani hapa na kuanza majukumu yangu mapya takribani mwezi mmoja uliopita kwa kweli sikuridhishwa na hali ya usafi wa mazingira haya ya ofisi .....nimelazimika kuanza usafi kwanza hapa ofisini kwangu maana ni hatari hata kwa usalama kama nyoka na wadudu wengine...hii ni serikali ya hapa kazi Tu hivyo kama mheshimiwa rais wetu mpendwa Dr John Magufuli alishiriki mwenyewe usafi hivyo ni lazima kila mmoja kuonyesha kuunga mkono kwa vitendo na sitaacha kuchukua hatua kwa wote watakaoshindwa kufanya usafi ,”
Bi Asia alisema kuwa kutokana na zoezi hilo kuwalenga wananchi wote kwa kila mmoja kufanya usafi katika eneo lake analo ishi kwa upande wake hakuona sababu ya kuanza kuhamasisha wananchi kufanya usafi kwenye mazingira ambayo yanawazunguka wakati mazingira yanayozunguka ofisi yake mkuu wa wilaya kuwa machafu hivyo alilazimika kuhamasisha wakuu wa idara na walimu pamoja na wanafunzi kufika kusaidia kuweka mazingira safi katika ofisi hiyo.
Pia alisema atawashauri madiwani kutunga sheria ndogo za usafi wa mazingira itakayotumika kuwawajibisha wananchi watakaoshindwa kufanya usafi katika maeneo yao na kwa kuanza anawataka wananchi wote wa wilaya ya Kilolo kuacha tabia ya kupanda mahindi kando ya nyumba zao kwani ni hatari kwa usalama wao .
Hata hivyo alisema utamaduni wa wananchi kushiriki uchafu umekuwa ni mdogo sana katika wilaya hiyo hasa ukitokana na mazoea yakutoshirikishwa zoezi hilo la usafi ambalo alisema kwa sasa usafi wa mazingira si kujitakia tena ni lazima kwa wananchi wote kufanya usafi katika maeneo yao kila jumamosi ya mwisho kwa kila mwezi na atakayepuuza atawajibika kwa mujibu wa sheria .
Baadhi ya wananchi walioshiriki usafi katika ofisi hiyo ya mkuu wa wilaya walieleza kufurahishwa na hatua ya mkuu huyo wa wilaya kuonyesha mfano wa vitendo kwa kuanza usafi katika mazingira yanayozunguka ofisi yake ambayo yalikuwa ni machafu zaidi ukilinganisha na mazingira yanayozunguka ofisi nyingine ama makazi ya wananchi.
Salome Kikoti ni mkazi wa Lugalo alisema kuwa mwonekano wa mazingira ya ofisi ya mkuu wa wilaya yalikuwa ni mabaya zaidi na kuwa hata watumishi wa ofisi hiyo walikuwepo hatarini kung'atwa na nyoka .
"Leo wakati tunafanya usafi wa kufyeka nyasi na vichaka katika eneo hili la ofisi ya mkuu wetu wa wilaya tumeua nyoka mmoja hii ni dalili ya wazi kuwa kuendelea kuviacha vichaka hivi na uchafu katika mazingira haya ya ofisi ya mkuu wa wilaya ilikuwa ni kukaribisha nyoka kuweka makazi yao eneo hili "
Pamoja na mkuu huyo wa wilaya kufanya usafi katika ofisi yake pia alishiriki kufanya usafi Zahanati ya Kilolo ,shule ya msingi Kilolo na katika maeneo ya biashara ya wananchi wa Luganga Kilolo .
Toa Maoni Yako:
0 comments: