Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Sophia M. Simba (Mb.) akikata utepe kuzindua Kitini cha Zana za Mawasiliano kuhusu Elimu ya Malezi kwa Familia, kushoto kwake ni Mhe. Dk. Pindi H. Chana (Mb) Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, kulia kwake ni Georgina Mtenga kutoka UNICEF na Anna T. Maembe Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
Waziri akionesha Kitini hicho kwa Wazazi, Watoto, Waandishi wa Habari na Taasisi mbalimbali katika Mkutano huo.

Picha zote na Hassan Mabuye
---
Na Erasto T Ching’oro- Msemaji Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Familia inayoadhimishwa tarehe 25 Mei, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Sophia M. Simba (Mb) amezindua Kitini cha Elimu ya Maelezi kwa Familia Kuzuia Ukatili dhidi ya Watoto katika familia na jamii kwa ujumla.

Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Familia huadhimishwa kila mwaka tarehe 15 Mei kulingana na Tamko la Baraza la Umoja wa Mataifa Na. 47/237 la mwaka 1993. Tamko hili linahimiza nchi wanachama wa Jumuiya ya Umoja wa Mataifa kuwa na siku maalum ya familia ili kutafakari masuala yanayoikabili familia na kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto zilizopo.

Waziri Simba ameeleza kuwa huu, Tanzania itaadhimisha siku hii katika mikoa na wilaya. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Familia 2015 ni: “Usawa wa Kijinsia na Haki za Watoto katika Familia: Wanaume Wawajibike”. Kauli mbiu hii inawakumbusha wanaume kutambua wajibu wao katika kuhudumia familia na kuachana na aina zote za ubaguzi wa kijinsia na kuwapatia watoto haki zao za msingi.

Katika kuenzi siku hii, Wizara Simba amezindua Kitini cha Elimu ya Maelezi kwa Familia Kuzuia Ukatili dhidi ya Watoto katika familia, tukio ambalo ujumbe wake unaendana na kauli mbiu ya siku ya familia mwaka 2015. Kitini hiki kinatoa elimu ya malezi kwa wazazi na walezi kuzuia ukatili dhidi ya watoto. 

Uzinduzi wa Kitini hicho umefanyika mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na wawakilishi wa Baraza la Watoto wa mkoa wa Dodoma, Viongozi wa Serikali, viongozi wa asasi za kiraia, wazazi na walezi.

Waziri Simba alieleza masikitiko yake kuona kuwa kufikia karne hii bado ukatili dhidi ya wanawake, watoto na watu wenye ulemavu unaendelea kuripotiwa katika jamii yetu. Wanawake wanafanyiwa vitendo vya kikatili na wenzi na hata kuuwawa. 

Aidha, watoto nao wanafanyiwa vitendo vya kikatili kama vile kubakwa, kunajisiwa, kupigwa, kuchomwa moto, kukeketwa na kuozeshwa katika umri mdogo. Na kibaya zaidi, wenzetu wenye ualibino wamekuwa wahanga wa kukatwa viungo na kuuwawa katika familia zetu. Katika hali kama hii lazima sisi sote kulaani na kukemea ukatili.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: