Je una mtaji mdogo kama laki 5 mpaka milioni 1 hivi na unatafuta biashara yenye uwezo wa kukupa uhuru wa kipato kabisa?
Usikubali kubakia kwenye maisha hayo hayo kila siku na kila mwaka.
Usikubali kubaki kwenye ajira unalipwa laki 5 kwa mwezi sawa na Tsh 1,850 yaani dola moja kwa saa. Ina maana umesoma mpaka chuo kikuu halafu thamani ya lisaa lako moja ni $1 tu!!!!? Ndiyo maana watu wengi waliosoma sana huwa hawawezi kuwa matajiri kwa sababu wanauza muda wao kwa "bei chee" halafu siku zinazidi kuyoyoma haoni mafanikio. Huku tena ana mkopo wa gari nk. Makato na marejesho... Kwa nini usife masikini kwa style hiyo.?
Shida ni kwamba watu wanaabudu sana kuajiriwa wako tayari watoe hata rushwa ya ngono (kwa wadada) ili tu eti wajiriwe. Ajira imekuwa kama Mungu kwa wengine.
Wanafunzi vyuoni wanasubiri kwa hamu kumaliza shule ili wakaajiriwe reception kupokea simu na kukaribisha wageni.. Seriously?? Halafu unasema umasikini unasababishwa na sijui CCM sijui Escrow sijui Kikwete hivi unajitambua kweli. Sasa hivi mnapost vikatuni vya #ShemejiUnatuachaje?
Hujui mtumaini cha shemeji hufa fukara kabisa. Sikia... maisha bora ni maamuzi yako binafsi. Hapo ulipo kuna watu wanakuuzia vitu kila siku.. Wewe unauza nini. Ndiyo unaamua kuuza muda wako kwa bosi wako. Halafu unashangaa watakuja UKAWA na miaka 10 ijayo hutakuwa na nyumba Masaki bado wala hutaweza kusomesha watoto wako shule bora wala hutaweza kusafiri ukapumzike na familia Hawaii.
Bado utakuwa unakula ugali dagaa wali njegere siyo unapenda ila ndo itakavyokuwa. Dont sell time for money. You will die poor. Utakaaje mwezi mzima ulipwe laki moja na nusu halafu unatumia vocha ya elfu 50 kuja Facebook kulaumu serikali na kumsifia Wema Sepetu ambaye hakujui hata. Watoto wako watakula comment zako au? Change today. Usipobadilika utakufa maskini!
Chukua hatua mpya ili upate matokeo mapya!
Acha wanaolalamika waendelee kulalamika. Acha wanaolalamika kukosa wazazi waendelee kulaumu bali wewe chukua hatua mpya!
Bill Gates anasema: "KAMA ULIZALIWA MASKINI HILO SIYO KOSA LAKO, LAKINI KAMA UKIFA MASKINI HILO NI KOSA LAKO"
Unafikiri uongo?
Tukiandika mambo kama haya wengine wanatuona wajinga!
Chukua hatua ndugu jifunze biashara unayoweza kuanza kwa laki 5 tu na ikabadili kabisa maisha yako! Kama huna tafuta.
Kumbuka tena maisha ni ya kwako na ni WEWE utakayeyabadili! Lowassa, Dr Slaa, Prof Lipumba hawawezi kukufanya wewe uhamie Oysterbay. Kila Mei Mosi raisi huwa anaongeza mishahara kwa wafanyakazi. Kwani ndiyo wamekuwa na maisha bora tayari? Jiulize maswali ya msingi. Mwajiri hawezi Kukubadirishia maisha.



Toa Maoni Yako:
0 comments: