Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Ummy Mwalimu (kushoto) akionyesha moja kati ya simu 350 zilizotolewa na Kampuni ya Tigo kwa ajili ya mkakati wa usajili wa watoto waliozaliwa wenye umri chini ya miaka mitano kwa njia ya simu kwa kutumia mtandao wa Tigo,wakati wa uzinduzi uliofanyika Mkoani Mwanza jana, kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Ali Maswanya, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa usajili,ufilisi na udhamini (RITA) Emmy Hudson na Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (aliyevaa miwani).
---
Kampuni ya Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Wakala wa Usajiri, Ufilisi na Udhamini yaani RITA, Shirika linalohudumia watoto ulimwenguni UNICEF na wadau wengine jana wamezindua awamu ya pili ya usajiiri wa kuzaliwa kupitia mfumo wa simu za mkononi, hii ikiwa na lengo la kuharakisha katika kuongeza idadi ya watoto wenye chini ya umri wa miaka 5 walio na vyeti vya kuzaliwa.

Akizungumza wakati wa sherehe, Maneja wa Tigo Kanda ya Ziwa Bw. Ally Maswanya alisema kuwa huduma hii inawawezesha wazazi kusajiri vizazi vipya pamoja na wale wenye Watoto chini ya miaka mitano kupitia ujumbe mfupi yaani SMS-hii ni sawa na huduma ambayo inaweza kupatikana kwenye simu yoyote ya mkononi .

Kama kampuni ilivyo na dhamira ya kutumia njia bunifu katika kusaidia jamii inayotuzunguka, tunajisikia fahari kutoa msaada kwa RITA na wadau wengine katika mchakato wa kuwapa watoto utambulisho – ambao ni haki yao ya kuzaliwa. Tigo inayofuraha kwa kuchangia katika mpango ambao unaleta haki za msingi kwa watoto wote - kutambua rasmi uwepo wao na utaifa wao. Kitu ambacho kinahitajika kwa mzazi ni kutumia simu ya mkononi tu kusajiri jina na tarehe ya kuzaliwa, "alisema.

Mfumo huu wa usajili wa kuzaliwa unatumia teknolojia bunifu ya Tigo kupitia simu za mkononi. Huduma hii kupitia simu za mkononi inarahisisha mchakato wa usajili wa kuzaliwa kwa kuingiza taarifa za usajili katika simu ya mkononi ambayo hutuma taarifa hizo makao makuu ya RITA kwa muda muafaka. Huduma hii imetengenezwa ili kufanya kazi kwenye simu za mkononi na mifumo ya uendeshaji ya aina yoyote.

Kwetu sisi kuendelea kutoa huduma kwa Watanzania, ni muhimu kwa serikali kuwa na takwimu sahihi juu ya idadi ya watu ikiwa ni pamoja na idadi ya watoto wanaozaliwa. Tunaamini kwamba kwa kutumia teknolojia ya simu za mkononi katika kusajili watoto na kutoa vyeti vya kuzaliwa italeta tija sio tu kwa walengwa lakini pia kusaidia kasi ya maendeleo ya jamii, "alisema Angela Kairuki, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria.

Uzinduzi wa mpango huu unaendana vizuri na mkakati wa RITA wa kuhakikisha Watanzania wote wanaozaliwa wanapata usajili, kitu ambacho ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya nchi ," alisema Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Bi Emmy Hudson.

Naibu mwakilishi wa shirika la UNICEF Tanzania Bwana Paul Edwards, alipongeza Serikali ya Tanzania kwa dhamira yake ya kuweka kipaumbele haki za mtoto. Kama wenzi wa maendeleo, tunakaribisha mpango ambao utawapatia watoto haki zao za msingi za kusajiliwa. Programu hii itasaidia katika maeneo mengi ambapo watu wameshindwa kupata usajili kwa sababu mbalimbali, "alisema Bw Edwards.

Leo ni hatua nyingine katika ushirikiano kati ya Serikali ya Canada na Tanzania katika kushughulikia afya ya mtoto na uzazi," alisema Catherine Addison, Afisa Maendeleo Mwanandamizi wa DFATD Canada. Tunalenga kuwa na watoto angalau 400,000 walio na umri chini ya miaka mitano watakaokuwa wanapatiwa vyeti vya kuzaliwa katika Kanda ya Ziwa ifikapo Desemba mwaka 2015, "aliongeza.

Tumefurahi kuwa sehemu ya mradi huu wenye lengo la kuwa na uzazi wenye ufanisi na mfumo wa usajili wa raia ambao ni sehemu muhimu katika kusaidia kasi ya maendeleo ya jamii," mwakilishi wa nchi za nje wa huduma za kujitolea (VSO) alihitimisha.

Wakati wa tukio hilo ilibainika kuwa katika kipindi cha miezi sita tu Kampuni ya Tigo Tanzania, kwa kushirikiana na shirika linalohudumia watoto la UNICEF, wakala wa usajiri RITA na wadau wengine wametoa ulinzi kwa zaidi ya watoto 100,000, nafasi muhimu katika jamii na ufunguo wa maisha yao ya baadaye, kwa msaada wa program hii mpya ya simu za mkononi. Mkoa wa kwanza kufurahia huduma hii ulikuwa ni Mbeya, ambapo mpango ulizinduliwa mwezi Julai mwaka 2013.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: