Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi akisoma hotuba yake kabla ya kufunga rasmi mkutano wa Wadau wa Sekta ya ujenzi nchini uliondaliwa na Bodi ya Wakandarasi nchini CRB ikishirikiana na Bodi ya Wahandisi ERB pamoja na Bodi ya AQRB.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akizungummza katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi (CRB) Eng. Consolata Ngimbwa akimkabidi zawadi mgeni rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi kama ishara ya kutambua mchango wake katika maendeleo ya sekta ya ujenzi nchini.
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi akimkabidhi cheti cha ushiriki kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe kabla ya kufunga mkutano huo.
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wengine akiangaalia moja ya vifaa vya ujenzi katika maonesho ya wadau wa sekta ya ujenzi nchini.
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi akikagua aina mbalimbali za mbao zinazotumika katika utengenezaji wa samani hapa nchini.
Washiriki wakimshangilia Rais Mstaafu Mzee Mwinyi kabla ya kuanza kutoa hotuba yake.
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Ujenzi
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na baadhi ya watumishi wa wizara ya Ujenzi kabla ya kuanza kwa mkutano wa CRB. Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi


Toa Maoni Yako:
0 comments: