Mkutano ukiendelea.
 Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mkutano wa amani, umoja na utulivu wa nchi utakaofanyika kuanzia leo na kesho ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa, serikali, dini, asasi za kiraia na wazee. Kulia ni Msaidizi wa mkurugenzi huyo, Gallus Abedi na Ofisa Mipango, Edger Atubonekisye.
---
MKURUGEZI Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku amEsema taasisi hiyo imeandaa mkutano wa mashauriano utakao wakutanisha viongozi wakuu wa Serikali, viongozi wa dini pamoja na viongozi wa kisiasa kujadili hali ya amani nchini.

Akizungumza  jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa za mkutano huo kwa vyombo vya habari Butiku alisema lengo kuu la mkutano huu ni kujadili viashiria vya uvunjifu wa amani na kupata shuluhisho ambalo ni kutunza amani chini.

''Lengo kubwa la mkutano huu ni kuwakutanisha viongozi wakuu wa Serikali, siasa na viongozi wa dini ili kujadili na kushauriana kuhusu suala zima la kulinda na kutunza amani na utulivu wa nchi yetu, ''alisema.

Butiku alisema kumekuwepo na viashiria vingi vya uvunjifu wa amani nchini kama vile mauaji ya walemavu wa ngozi, migogoro ya ardhi inayosababisha vurugu katika baadhi ya maeneo na ubishi kuhusu kuwepo kwa muungano.

''Tumewaalika viongozi wakuu katika tasisi mbalimbali wakiwemo pia viongozi wa dini kwasaba viongozi ndio wanaohusika kikamilifu kulinda amani umoja na utulivu  wa nchi yetu,''alisema.

Alisema viongozi wanao wajibu wa kuelewa,kutambua na kuchukua hatua sitahiki dhidi ya kulinda na kutunza amani na umoja wa nchi hii.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: