
Na Mwandishi Wetu
Mabondia Iddi Pialali wa Kiwangwa Bagamoyo na Adam Ngange wa Chanika Dar es salaam watapima uzito siku ya ijumaa katika stendi kuu ya mabasi Bagamoyo na kupigana siku ya jumamosi ya mei 16 katika ukumbi wa che kwa che uliopo Bagamoyo mjini ambapo mabondia hawo watamalizia ubishi wao wa nani zaidi kati ya bagamoyo na Chanika
Mpambano uho utakaosimamiwa na chama cha ngumi za kulipwa P.S.T litakuwa la raundi sita na kg 61 ambapo kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi siku hiyo yatakayowakutanisha bondia
Rashidi Haruna atakumbana na Kaminja Ramadhani na Harid Hongo atakabiliana na Kishoki Mbishi mpambano mwingine ni Abdallah Samata atakaye zidunda na Maono Alli
Mipambano hiyo inaletwa kwenu na Sharif Promotion wakati mgeni rasmi siku hiyo ni bondia kutoka morogoro Cosmas Cheka ambaye atakuja kuwapa nasaa mbalimbali mabondia na mashabiki wa mchezo wa masumbwi kuweza kusonga mbele kwa mchezo huo mjini Bagamoyo.


Toa Maoni Yako:
0 comments: