Mwenyekiti wa kijiji Cha Mavanga Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema )akimpongeza mbunge Filikunjombe kwa misaada yake.
Paroko wa kanisa la Anglicana kushoto akipokea msaada wa bati 300 kutoka kwa mbunge Deo Filikunjombe.
Mbunge Filikunjombe kati akikabidhi saruji kwa ajili ya shule ya msingi kijiji cha Mavanga.
Mbunge Filikunjombe akikabidhi kitanda cha wanawake wajawazito kujifungulia.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mavanga Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema )akiwa amepokea msaada wa Darubini toka kwa mbunge Deo Filikunjombe.
Mbunge Filikunjombe akimkabidhi mpira kijana wa Chadema kijiji cha Mavanga.
Wananchi Mavanga wakimkabidhi zawadi ya kuku mbunge wao Filikunjombe.
Mbunge Filikunjombe akipokea zawadi ya mbuzi toka kwa vingozi wa kanisa la Anglicana baada ya kuwasaidia bati 300 za ujenzi wa kanisa.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mavanga Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema )akimongeza mbunge Filikunjombe.
Filikunjombe akizungumza na mlemavu aliyefika katika mkutano wake.
Wananchi wa kijiji cha Mavanga wakiwa wamembeba mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe.
Mbunge Filikunjombe akicheza mpira na wanafunzi hao baada ya kuwapa msaada wa mpira na sukari kwa mwaka mzima.
Katibu mwenezi mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya akishiriki kucheza ngoma.
Mbunge Filikunnjombe na katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe Bw Mgaya wakicheza ngoma
---
Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe asema baadhi ya wabunge ,mawaziri na watendaji wabovu serikalini wanakichafua chama cha mapinduzi ( CCM ).
Filikunjombe alisema kuwa Ccm ni chama makini na kinachopendwa sana ila shida ipo kwa baadhi ya watu waliopo ndani ya Ccm na serikali ni bomu.
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo leo katika kijiji cha Mavanga wakati akijibu maswali ya wananchi na viongozi wa vyama vinavyounda katiba ya wananchi (Ukawa) kuhusiana na Ccm kuwateulia wananchi viongozi wasio na sifa kugombea nafasi mbali mbali.
Alisema kama kila mmoja angetimiza wajibu wake katika nafasi yake hakuna mpinzani ambae
angechaguliwa ila kuchaguliwa kwa wapinzani ni kushindwa kwa wale waliowaamini kutoka Ccm kushindwa kuwajibika kwa wananchi waliowaamini.
Filikunjombe alisema atakuwa mbunge wa mwisho kunyoshewa kidole na watanzania wakiwemo wananchi wake wa Ludewa kwa kushindwa kuwatumikia wananchi na chama chake cha CCM.
Kwani alisema hakuomba ubunge kwa ajili ya kujinufaisha binafsi ila aliamua kugombea ili kuwatumikia wana Ludewa kwa kuwapelekea maendeleo hivyo Kazi Yake kwa sasa hadi mwisho wa ubunge wake ni kuleta maendeleo kwa wananchi wake na kuona ahadi zake zinatimia kwa muda uliopangwa na si kujinufaisha kwa wakati.
Akielezea msaada huo wa vitu mbali mbali vyenye thamani ya Tsh milioni 40 alivyotoa alisema ni pamoja na kitanda cha kujifungulia wajawazito chenye thamani ya Tsh milioni 5.2,Darubini ,pesa ya taslimu Tsh milioni 1 bati zaidi ya 500 ,rangi debe 20 ,saruji zaidi 525 na vifaa vingine vingi kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa miradi mbali mbali ya kijiji na ujenzi wa makanisa, shule na wodi la wazazi
"Toka Filikunjombe ameingia madarakani mwaka 2010 na kuwepo kwa kasi ya maendeleo ndio tunashuhudia wana Ludewa wakirejea Nyumbani na kujitangaza kuwa wao ni wakazi wa Ludewa tofauti na zamani wengi walikuwa wakijificha kwa aibu "


Toa Maoni Yako:
0 comments: