Mkuu wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Sebo (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu tamasha lijulikalo kama Komaa Concert  litalofanyika mwishoni mwa mwezi mei  kwa ajili ya kuadhimisha miaka 16 ya muziki ya msanii Juma Nature 'maarufu Kiroboto' namna ya kuonesha kuthamini mchango wake katika muziki wa bongo fleva na kuwakumbusha watanzania juu ya safari ya muziki wa Tanzania kwa ujumla. Kulia ni mwanamuziki huyo, Juma Nature na Ofisa Habari wa kituo hicho cha redio, Lydia. Moyo.
---
Na Dotto Mwaibale

KATIKA kusherehekea miaka 16 ya muziki kwa msanii Juma Nature, Kituo cha Radio cha EFM, wanatarajia kuungana nae kwenye sherehe hizo.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Mahusiano Denis Sebo alisema wao ni wadau wa muziki na pia wanatambua mchango wa wasani wakongwe nchini ikiwa ni pamoja na Juma Nature.

"Leo tuna furaha kutangaza kwamba wakati Juma Nature anatimiza miaka kumi na sita kwenye game ya muziki, sherehe zake zimeunganishwa na zakwetu ili kwapamoja tufanye concert kubwa kusherekea miaka 16 ya Juma Nature," alisema Sebo.

Alisema tamasha hilo lijulikanalo kama 'Komaa Concept' ambalo litafanyika mwishoni mwa Mei,  mwaka huu kwa ajili ya kuadhimisha miaka 16 ya muziki ya msanii Juma Nature, maarufu kama 'kiroboto'.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: