Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli, akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara yake(hawapo picha) kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 10 ya Serekali ya awamu ya nnne katika sekta ya ujenzi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe, akihutubia wafanyakazi wa Wizara hiyo(hawapo pichani) katika Baraza la Wafanyakazi la Wizara lililofanyika leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi na Umeme Dkt. Wiliam Nshama wakwanza kushoto akiwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Elizabeth Tagora, pamoja na Mkurugenzi wa Barabara Eng. Ven Ndyamukama pamoja na baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli, katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara kilichofanyika leo jijini Dar es salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) Elius Mwakalinga (wa kwanza kulia) akisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (hayupo pichani) katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi lililofanyika jijini Dar es salaam. Wa Pili kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Bi. Marcelin Magessa
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi la Wizara ya Ujenzi wakifurahi jambo katika kikao cha Baraza hilo.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Taasisi na vitengo vilivyo chini ya Wizara katika Baraza la wafanyakazi lililofanyika jijini Dar es salaam. Wa tatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng. Musa Iyombe. Picha zote kutoka Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Ujenzi.


Toa Maoni Yako:
0 comments: