Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, akikata utepe kufungua maonyesho ya uwekezaji katika majengo yajulikanayo kama Dar Property Expo kwenye ukumbi wa VIP wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Jumamosi Mei 2, 2015. Makampuni na mabenki mbalimb ali yanashiriki kwenye maonyesho hayo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi alipotembelea banda la Dege Eco Village katika maonyesho ya uwekezaji majengo yajulikanayo kama Dar Property Expo kwenye ukumbi wa VIP wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Jumamosi Mei 2, 2015.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akipata maelezo alipotembelea banda la Dege Eco Village katika maonyesho ya uwekezaji majengo yajulikanayo kama Dar Property Expo kwenye ukumbi wa VIP wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Jumamosi Mei 2, 2015.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege Eco-Village akibadilishana mawazo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi alipotembelea banda la Dege Eco Village katika maonyesho ya uwekezaji majengo yajulikanayo kama Dar Property Expo kwenye ukumbi wa VIP wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Jumamosi Mei 2, 2015.
Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Dege Eco -Village Bw. Adam akiongea na waandishi wa habari kufafanua jambo.
Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Dege Eco -Village Bw. Adam akimpa maelezo mwenzake.
Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick ametoa wito kwa Makampuni mbalimbali kujenga nyumba nje ya Miji kwa ajili ya kuhakikisha wanapunguza msongamano wa watu Mijini.
Akizungumza katika maonyesho ya Nyumba na Vifaa vya Ujenzi yanayoendelea kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Sadick alisema kuwa wadau mbalimbali wanatakiwa kuchamkia fursa hiyo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wanapunguza idadi ya watu wanaoishi katikati ya Miji.
Alisema kuwa pia Makampuni mbalimbali yanatakiwa kujenga nyumba zenye ubora na kuziuza kwa bei ya chini ili kupata wateja wengi zaidi.
Alisema kuwa Serikali inatarajia kujenga na kukarabati barabara zote ambazo zipo pembezoni mwa Miji kwa ajili ya kuhakikisha shughuli hiyo inafanyika bila kipingamizi.
“Makampuni yanatarajiwa kuanza kujenga nyuba katika maeneo ya nje ya Miji kwa ajili ya kupunguza msongamano wa watu ambao upo katika Miji mikubwa,” alisema.
Afisa Masoko wa Kampuni ya Dege Eco Village, Adam Jusab, alisema kuwa wamefanikiwa kujenga nyumba katika eneo la Kigamboni ambazo zipo katika hatua ya mwisho kukamilika.
Alisema wamejenga jumla ya nyumba 7410 mpaka sasa ambapo baada ya mradi huo kukamilika 2018, wanatarajia kwenda kujenga nyumba zingine Mkoa wa Arusha.
Alisema kuwa wameshapata eneo Arusha lenye heka 2000 ambapo zoezi la ujenzi litaanza mwaka 2018.
“Tunatarajia kumaliza ujenzi 2018 ambapo tutaanza Mkoa wa Arusha kwa kuwa tumeshapata eneo na ramani imeshachorwa,” alisema.
Alisema pia maonyesho hayo yanawasaidia kupata wateja zaidi ambao wanakuwa hawana uwezo wa kufika katika ofisi zao kwa ajili ya kutoa oda ya kujengewa nyumba.



Toa Maoni Yako:
0 comments: