* Kuna Dada mmoja Alichumbiwa na watu Wanne
1. Msanii
2. Mvuvi
3. Afande
4. Doctor .
Siku moja Dada huyo alienda mtoni kufua nguo zake ghafla alitokea Mamba akamchukua akazama nae Majini pale pale.
MSANII: Akatunga Wimbo akaanza Kumwimbia Mamba mamba akatokeza Kichwa juu.
AFANDE: Pale pale akampiga Mamba Risasi akafa na Dada alibaki akitapatapa ndani ya maji pale pale.
MVUVI: Akaogelea kwenda kumuokoa akamleta Nchi Kavu pale pale.
DOCTOR: Akamtibu Majeraha mpaka akapona.
Swali linakuja! Je ni nani anaye stahili kumuoa kati ya watu hao Wanne?.



Toa Maoni Yako:
0 comments: