Afisa wa Huduma kwa Wateja wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Gladys John katikati akichagua koponi ya mmoja wa washindi wa shindano la Kopa Bayport linaloendelea ambapo washindi watatu wamepatikana na kila mmoja kupata bahati ya kujinyakulia Sh Milioni moja kila mmoja baada ya kukopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz. Kulia ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport, wakati kushoto ni Humud Abdulhussein, Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.
Tunatafuta washindi wa kujinyakulia Sh Milioni moja kila mmoja kwa washindi watatu kutoka Bayport Financial Services. Ndivyo wanavyoonekana kusema katika droo hiyo ambapo washindi kutoka Njombe, Dar es Salaam na Bukoba wamechanua.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SHINDANO la Kopa Bayport kwa njia ya mtandao linaloendeshwa na taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, limezidi kuchanja mbuga, baada ya wateja watatu wa mwezi Mei kuibuka na Sh Milioni moja kwa kila mmoja, huku mikoa ya Bukoba, Njombe na Dar es Salaam ikichanua katika droo iliyochezeshwa jana, jijini Dar es Salaam.
Wateja hao walioshinda katika shindano hilo ni Tryphone Mashamba mkoani Njombe), Kisa Mboya (Dar es Salaam) na Oscar Gadawu (Bukoba) ambao wote kwa pamoja wameibuka na Sh Milioni moja baada ya kukopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz, ikiwa ni huduma nzuri kutoka kwenye taasisi hiyo ya Bayport Financial Services.
Akizungumza katika droo hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema shindano lao limepokewa vizuri na wateja wao, waliopata urahisi wa upatikanaji wa huduma za mikopo kutoka kwenye taasisi hiyo.
Alisema awali wateja walilazimika kusafiri kuelekea kwenye tawi lao, lakini kuanzishwa kwa tovuti hiyo, kumetoa urahisi wa ukopaji kwa kiasi kikubwa mno, huku kila mmoja akiwa na uwezo wa kushinda endapo ataamua kutumia huduma hiyo.
Naye Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Humud Abdulhussein, alisema promosheni hiyo ya kopabayport ni nzuri kwa wateja na Watanzania wote wanaoweza kujikwamua kwa kupata mikopo isiyokuwa na dhamana wala amana kutoka Bayport.
Naye Meneja Huduma kwa Watejanwa Bayport Financial Services, Gladys John, aliwataka watanzania kuendelea kuiunga mkono Bayport kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi kutokana na fursa mbalimbali za mikopo isiyokuwa na amana wala dhamana, bila kusahau Kopa Bayport inayoendelea kutolewa kwa ajili ya kuwapongeza wanaomua kutumia huduma hiyo nzuri.


Toa Maoni Yako:
0 comments: