Afisa masoko wa Airtel tanzania Prospa Mwanda akionyesha kwa wanafunzi wa chuo Kikuu dodoma (UDOM) jinsi huduma mpya ya Airtel Wi-Fi Intaneti inavyofanya kazi mara baada ya uzinduzi wa huduma hiyo chuoni hapo jana. Airtel Tanzania chuoni hupo imezindua huduma ya UNI Wi-Fi Intaneti yenye ubora zaidi na itakayopatikana kwa wananfunzi kwa gharama nafuu
Meneja masoko wa Airtel Uni Wi-Fi Bi Aneth Muga anaepiga picha ya selfie ili waitume kwa kutumia huduma ya Airtel Wi-Fi intaneti kwa baadhi ya uongozi wa wanafunzi na mshauri wa wanafunzi chuoni hapo mara baada ya Airtel kuzindua huduma yao ya intaneti Wi-Fi yenye kasi zaidi maalum kwa wanafunzi wa chuo hicho jana.
Mshauri wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) bw, Dick Manong akiongea na wanafunzi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel UNI Wi-Fi jana chuoni hapo ambapo itawasaidia wanafunzi kupata intaneti kwa gaharama nafuu ya yenye kasi zaidi.
---
• Pia Airtel yazinduzi mnara wa pili UDOM
Dodoma, Aprili 27, 2015, kutokana na ukweli kwamba Dodoma ni mji mteule na wenye kuendelea kwa kasi hapa nchini na pia ni mji uliobahatika kuwa miongoni mwa mji wenye chuo kikubwa hapa Tanzania, Airtel Tanzania mkoani huko imezindua huduma ya UNI Wi-Fi Intaneti yenye ubora zaidi na itakayopatikana kwa wananfunzi kwa gharama nafuu.
UNI WI-FI itawezesha wanafunzi zaidi ya 60,000 katika Chuo Kikuu cha Dodoma kupata huduma ya kimtandao ya Intaneti iliyo bora na nafuu pamoja na kukidhi mahitaji ya wote waishio chuoni hapo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Airtel Bi , Adriana Lyamba alisema: "Leo hii tunazindua Airtel UNI WI- FI huduma ya internet inayopatikana kwa bei nafuu kwa ajili ya wanafunzi na pia tumeongeza mnara wa pili wa simu ambao tunaamini utaimarisha mtandao wetu hapa UDOM na kuinua uchumi wa nchi yetu na kwa watu wanaoishi karibu na maeneo haya "
Tunafuraha kubwa kwa Airtel kuweza kuboresha Maisha ya wanafunzi hapa chuoni kwani spidi hii itawawezesha wanafunzi kuweza kufanya utafiti wao, kupata habari mbalimbali za taaluma au kijamii kupitia mtandao wetu wa Airtel "
Meneja Masoko wa Airtel UNI WI-FI, Bi, Aneth Muga, alisema "Airtel wifi itakuwa inapatikana kwa mwanafunzi yoyote hapa UDOM, kwa kutumia simu zao za mkononi, laptop, kamera na kwa mwanafunzi yoyote aliyepo UDOM bila kujali mtandao wa simu wanaoutumia.
Wanaweza kununua UNI Wi-FI vocha ambayo inapatikana masaa 24 , kwa kifurushi cha siku , wiki, mwezi na kifurushi cha usiku mzima.





Toa Maoni Yako:
0 comments: